
MADIWANI watatu wa
chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) jimbo
la Iringa mjini wamemwandikia barua msimamizi wa
uchaguzi jimbo la Iringa mjini kujiuzulu nafasi zao
kuanzia leo Augosti 23 majira ya saa40 jioni
Wakizungumzia azma
hiyo ya kujiuzulu nafasi zao madiwani hao Baraka
Kimata wa kata ya Kitwiru na madiwani
wenzake wawili wa viti maalum Leah Mlelewa na Husna
Ngasi walisema kuwa wamefikia uamuzi huo baada
ya kuchoshwa na mwenendo wa chama hicho jimbo
la Iringa mjini na hivyo wameamua kuachia nafasi zao
na kubaki bila kuwa wanachama ama viongozi
wa chama hicho.
Kimata ambae alikuwa ni katibu
mwenezi wa chadema jimbo la Iringa mjini na
mwenyekiti wa madiwani jimbo la Iringa mjini alisema
nafasi zake zote ameziacha na kuwa kwa sasa
ataendelea na shughuli zake nyingine nje ya
siasa kwani siasa kwa ujumla wake imemshinda .
Kwani alisema pamoja
na kuwa chama chao ni chama cha Demokrasia
ila katika jimbo la Iringa mjini Demokrasia
imekuwa ikivurugwa na baadhi ya viongozi na
hata kupelekea madiwani kuona chama hichop
ni kichungu na hivyo hatua yao ya kujiuzulu ni
kilelelezo tosha kuwa ndani ya chama hicho Iringa
mjini hakuna usalama.
Alisema mbali ya
sababu nyingine zilizopelekea kujiuzulu kwake
na wenzake ila bado amekuwa akikosa
ushirikiano kutoka kwa mbunge wa jimbo mchungaji
Peter Msigwa ambae toka amechaguliwa kata
yake hajapata kufanya ziara ya aina yeyote
na hivyop kutokana na kubaguliwa huko na
pamoja na kuendelea kudidimizwa haki yake wakati
wa kuwania nafasi mbali mbali ikiwemo ya umeya na
unaibu meya ameona ni vema kutojihusisha na masula
la siasa .
" kumekuwepo na
maneno kutokana kwa watu kuwa tumenunuliwa
kwa ila ukweli utabaki pale pale tumeondoka kwa
kukwepa demokrasia mbaya ndani ya chama chetu
na tutakuwa huru kujiunga na chama chochote
kama ACT Wazalendo ama chama kingine chochote
chenye Demokrasia nzuri "
Kwa upande wake
Mlelewa ambae alikuwa ni afisa habari wa jimbo la
Iringa mjini na katibu wa baraza la vijana la Chadema
(BAVICHA ) na katibu wa madiwani alisema ameachia ngazi
nafasi zote ikiwemo ya udiwani kama wenzake
na sababu za kufanya hivyo ni ubabe ndani
ya chama hicho .
Husna Ngasi
alisema pamoja na sababu nyingine ameachia ngazi
kutokana na kubaguliwa kwa misingi ya itikadi zake
za dini na kuwa kwa muda amekuwa akinyanyapaliwa na
hivyo kuamua kukaa pembeni .
Kwa upande wake
msimamizi wa uchaguzi jimbo la Iringa mjini
Dkt Wiliam Mfere alipoulizwa na mwandishi wa matukiodaimaBlog
kwa njia ya simu jana jioni alisema kuwa
bado hajapokea barua ya kujiuzulu kwao kwani
hakuwepo ofisini na kuwa akipatatazitolea maelezo
No comments:
Post a Comment