Wednesday, August 23, 2017

Waathiriwa wa janga la moto Soko la Sido kuendelea kubaki ,Naibu Spika achangia Milioni kumi


Image result for picha za moto sido

Image result for picha za moto sido
Baada ya Soko la Sido kuteketea kwa moto,hatimaye Serikali Mkoani Mbeya imeridhia Waathirika wa janga la Moto katika soko hilo kuendelea kubaki katika maeneo yao ya awali na kuagizwa kujenga  vyumba vya kudumu ili kukabilina na majanga ya moto yanapojitokeza.

Akitoa maelekezo ya serikali,Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla amewaagiza watendaji wa halmashauri kupiga kambi katika eneo la soko la Sido haraka kuanzia siku ya kesho, kwa ajili ya kubuni michoro na mpangilio wa soko hilo ili wafanyabiashara waanze ujenzi na hatimae kuendelea na biashara zaoa kama kawaida.

Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa wilaya ya Mbeya Mjini,Mkoa ikiwa ni pamoja na mbunge wa Jimbo  Mbeya Mjini Mh.Joseph Mbilinyi pamoja na Naibu Spika Mhe.Dkt Tulia Ackson ambaye ametoa msaada wa shilingi milioni 10 kwa wathirika hao.Aidha baada ya kutolewa kwa kiasi hicho cha fedha ,Mkutano huo ukaridhiwa kuwa fedha hiyo ibaki kwa Mkuu wa Mkoa huku uongozi wa soko ukipanga matumizi ya fedha hiyo.

Hata hivyo mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh.Makala ameliagiza Jeshi la Zimamoto kuendelea kutoa elimu ya zimamoto,kusambaza vifaa vya kuzuia moto na kuchimba visima vya maji vya ziada katika masoko huku akiwataka viongozi wa ngazi zote za mkoa kuchukua tahadhari za moto kwenye masoko kutokana na ripoti kuonesha chanzo cha janga hilo ni mabaki ya moto uliotokea kwenye moja ya vibanda vya mamalishe waliokuwa ndani ya soko hilo.

No comments: