Tuesday, August 22, 2017

Waziri: Serikali itakikisha wanafunzi kuanzia elimu ya msingi wanapata elimu bora.

Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi,Profesa JOYCE NDALICHAKO amesema serikali inaendelea mipango ya utekelezaji wenye lengo la kuhakikisha wanafunzi kuanzia elimu ya msingi wanapata elimu bora itakayowawezesha kumudu utumishi wa serikali,sekta binafsi na kujiajiri wenyewe.

Waziri NDALICHAKO ameyasema hayo Mjini Kasulu alipokuw akiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Grand High School,ambayo ujenzi wake ulikwama kabla ya wizara kutoa Shilingi BILIONI moja za kuendeleza.

Amesema pamoja na kutoa vifaa vya maabara katika shule zote za sekondari nchini, vyumba vya madarsa Elfu moja n 405 vimejengwa katika shule 378.

Kwa upande wo wananchi wameitaka serikali kuipa kipaumbele mikoa ya pembezoni ambayo ipo nyuma kwa kuongeza shule pamoja na vyuo.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma,Brigedia Jenerali mstaafu EMMANUEL MAGANGA akieleza kuwa Shilingi zaidi ya BILIONI 29 zitatumika hadi kukuamilisha ujenzi wa shule hiyo maalum.

No comments: