Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Rex Tillerson yuko mjini Beijing kufanya mazungumzo na viongozi wa China.
Ajenda kuu katika mkutano huo ni mzozo katika rasi ya Korea.
Marekani na Korea Kaskazini zimekuwa zikirushiana cheche za maneno katika miezi ya hivi karibuni
Utawala wa Trump unaamini China ina umuhimu mkubwa, katika juhudi za kuishurutisha Korea Kaskazini kusitisha uundaji wa silaha zake za Nuklia
China imeonyesha kujitolea kwake katika utekelezaji wa vikwazo vya Umoja wa mataifa dhidi ya taifa hilo.
Siku ya Alhamisi, Beijing ilitangaza kuwa mashirika ya Korea Kaskazini yanayoshirikiana na China hayana budi kufungwa.
Ziara ya Tillerson inakuja huku Rais Trump akitarajiwa kutembelea taifa hilo baadaye mwezi Novemba.
No comments:
Post a Comment