Na Mahmoud Ahmad Arusha
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli
amelipatia jeshi la Polisi Tanzania Milioni 260 kutokana na ajali ya
moto iliyotokea kwenye makazi ya polisi Arusha September 27 Mwaka huu
majira ya saa moja na Nusu usiku.
Akizungumza na Waandishi ya Habari jana Inspecta Jenerali wa polisi
Tanzania IGP Simon Sirro ,alisema kuwa Rais Magufuli ametoa fedha
hizo kutokana ya ajali ya moto iliyotokea jana na kusababisha familia
za askari wa polisi 14 na zenye wakazi 44 kupoteza mali na makazi ya
kuishi.
Sirro alisema kuwa Jeshi polisi Tanzania imetoa kiasi cha shilingi
milioni 40 kutoka kwenye mfuko wa Jeshi hilo ili kusaidia kujenga
makazi mapya ndani ya mwezi Mmoja na kuzipatia milioni moja kila
familia ya askari hao ili kuweza kujikimu kimaisha.
“Rais ameagiza wakala wa Taifa wa majengo { TBA} kuwapatia askari
makazi mpaka hapo ujenzi utakapokamilika ndipo waweze kurejea kwenye
makazi yao ya kudumu” alisema Sirro
IGP Sirro amewasisitiza Askari polisi kuwa ajali hiyo iliyotokea ni
kama ajali zingingene hivyo waendelee kuwa na imani na serikali wakati
wanashughulikia jambo hilo kukamilika mapema ndani ya Mwezi mmoja.
Aidha kamanda Sirro amewaomba Raia wema na Taasisi za Watu Binafsi
kujitokeza kutoa msaada kwa wahanga wa tukio la kuunguliwa na nyumba
zao na kupoteza mali zao zenye thamani kubwa.
No comments:
Post a Comment