Soko la kimataifa la zao la ndizi linatarajiwa kujengwa
wilayani Rungwe mkoani Mbeya lengo likiwa ni kuongeza kipato kwa wakulima wa
zao hilo na kuimua uchumi wa wilaya, mkoa na Taifa kwa ujumla.
Hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa wa Mbeya Bw. Amosi Makala
wakati wa ufunguzi wa kongamano la kutangaza fursa za uwekezaji mkoani mbeya
lililofanyika jijini Mbeya na kuhudhuriwa na viongozi na wadau mbalimbali wa
maendeleo kutoka ndani na nje ya mkoa pamoja na naibu Spika wa Bunge Dk. Tulia
Acson Mwansasu.
Aidha mkuu wa mkoa ameelezea fursa mbalimbali
zinazopatikana katika wilaya ya Rungwe na kuongeza kuwa viwanda vinavyotengeneza
vinywaji vinategemea gesi inayozalishwa katika halmashauri ya Busokelo na
Rungwe hivyo kuwataka wawekezaji kuendelea kuzitumia fursa hizo kwa manufaa ya
wananchi.
Kuhusu suala la uzalishaji wa Maziwa katika mkoa wa Mbeya
Mkuu wa Mkoa amezitaka wilaya zinazofuga Ng'ombe kwa wingi kuiga mfano bora wa
ufugaji wa ng'ombe wa maziwa kutoka Rungwe huku akiwataka wawekezaji kuwekeza
viwanda vya kusindika Nyama na Ngozi
katika wilaya ya Chunya ili waweze kufuga kisasa zaidi.
Katika kongamano hilo Makalla ameainisha fursa mbalimbali
za uwekezaji katika mkoa wa Mbeya na wilaya zake ikiwa ni pamoja na uwepo wa
madini, kilimo na ufugaji, na Vivutio vya utalii ambapo wilaya ya Rungwe
inavivutio vingi zaidi ukilinganisha na wilaya nyingine.
No comments:
Post a Comment