Wednesday, September 27, 2017

Tanzania yang'ara Umoja wa Mataifa

Waziri wa Mambo ya Nje, na Ushirikiano wa Afrika mashariki Augustine Mahiga amesema Tanzania imekuwa kivutio kikubwa katika viunga vya mkutano wa Umoja wa Mataifa kutokana na utendaji wa Rais Magufuli unaolenga kuwaletea huduma bora wananchi.

Akitoa Taarifa hiyo kutokea New York Dkt. Mahiga amesema kwamba katika mkutano wa 72 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kutokana na kuenea kwa sifa za utendaji wa serikali ya awamu ya tano.

"Nimekutana na wajumbe kutoka nchi za Afrika, Asia, Ulaya na Marekani na wengi wanasema nchi zao zipo tayari kumualika Rais Magufuli au viongozi wao wako tayari kuja Tanzania kupata uzoefu jinsi ambaavyo Rais anafanya mageuzi makubwa katika kipindi kifupi. Wanamuona ni mtu jasiri na mwenye upeo mkubwa katika kuwatumikia watu wake" Dkt. Mahiga
Ameongeza kwamba, Licha ya mpaka sasa kuhutubia kwenye baraza kuu la UN, nimeshafanya mikutano ya nchi na nchi au taasisi zipatazio 25 na wiki hii natarajia kufikisha mikutano 35.

Aidha Mahiga amesema pia mbali na sifa za Rais Magufuli uchache wa wajumbe walioongozana nae kwenda kwenye mkutano huo umekuwa kivutio kwani wengi wa watu wa mataifa mengine wameridhishwa na jinsi Tanzania inavyobana matumizi kwa kutumia vizuri pesa za walipa kodi ambao ni wananchi.

Balozi Mahiga ameungana na watu watatu kutoka katika Wizara yake pamoja na kuungana na Balozi kwenye umoja wa Mataifa Balozi Wilson Masilingi.

No comments: