Monday, October 23, 2017

Zimbabwe imekubali uamuzi wa WHO kumvua rais Mugabe ubalozi

Robert Mugabe

Haki miliki ya picha
Image captionBw. Mugabe mara nyingi husafiri ng'ambo kupata matibabu
Zimbabwe inasema imekubali uamuzi wa shirika la afya duniani kumvua rais Robert Mugabe wadhifa wa balozi mwema wa shirika hilo.
Waziri wa mambo ya nje Zimbabwe Walter Mzembi ametaja uamuazi huo kama hasara kwa shirika hilo la Umoja wa mataifa.
"Ni makubaliano ya pande mbili. Kelele zinazotokana na mjadala huu hazina thamani. Kwa hakika ni WHO lililokuwa linanufaika kutokana na kutajwa jina la rais," Amesema Waziri Mzembi.
Akitangaza hatua hiyo ya shirika la WHO mkuu wa shirika hilo Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema katika taarifa "Nimesikiliza vizuri wale wote ambao wameelezea hisia zao."
Awali alikuwa ameisifu Zimbabwe kwa kujitolea kuboresha afya ya umma.
Lakini wakosoaji walisema kuwa mifumo ya afya nchini Zimbabwe iliporomoka nchini ya utawala wa Mugabe wa miaka 30.
Wafanyakazi mara nyingi hukosa kulipwa na madawa wakati mwingine hukosekana huku Mugabe mwenyewe mwenye umri miaka 93 akiwa anasafiri nje ya nchi kupata matibabu.
Bw. Tedros alisema ameongea na serikali ya Zimbabwe na kuamua kuwa kumvua Mugabe wadhifa huo ni kwa manufaa ya WHO.
Alisema anasalia kujitolea kufanya kazi na chi zote na viongozi wake kujenga huduma bora za afya.
Uteuzi wa Bw. Mugabe ulipatawa na shutuma kali, Serikali ya Uingereza, waziri mkuu wa Canada na mashirika mengine kadha pamoja na watumiaji wa mitandao ya kijamii ni kati ya wale ambao walikosoa uamuzi huo.
Kufuatia kukosolewa kutoka kwa mashirika ya haki za binadamu na kushangazwa kwa mataifa mengi wanachama, WHO haikuwa na lingine ila kufuata mpango wake wa kumvua Robert Mugabe wadhifa wa balozi wa nia njema.

No comments: