MAKAMU wa Rais mstaafu, Dk Gharib Mohammed Bilal amesema Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela iliyopo jijini Arusha, inaipasha Tanzania kutokana na kuzalisha watafi ti wenye hadhi ya kimataifa.
Dk Bilal, msomi aliyebobea katika fizikia ya nyuklia, alisema hayo mwishoni mwa wiki wakati akiwatuhumu vyeti wahitimu 83 wa Shahada za Uzamili (Masters) na Uzamivu (PhD) kwa wasomi wa chuo hicho.
Akiwatunuku wanafunzi hao katika mahafali ya nne ya chuo hicho, alisema sasa Tanzania inapaswa kutembea kifua mbele kwa kuanza kuzalisha wataalamu watafiti wanaojulikana kitaifa na kimataifa.
Alisema taasisi hiyo inapaswa kupongezwa kwa kutoa wataalamu wagunduzi kwa ufadhili wa wataalamu wengine duniani na kuifanya Tanzania kuelekea kutimiza ndoto yake ya uchumi wa viwanda. “Hawa wataalamu wagunduzi wanatoka hapa watazalisha viwanda na kutoa ajira, hii ni furaha kubwa kwa nchi, kwani watasaidia viwanda vyetu pia kuoneka kutokana na ubobezi wao wa tafiti walizonazo,” alisema.
Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Karoli Njau alishukuru kwa kufanikiwa kupata ufadhili kwa baadhi ya wanafunzi wanaoandika maandiko mbalimbali. Alisema kwa sasa licha ya kuwa na tafiti mbalimbali, pia wanaendelea na utafiti mkubwa wa kuzalisha migomba na katika hilo wametafuta shamba wilayani Rombo ambako wanafunzi wao wanapelekwa kujifunza.

No comments:
Post a Comment