Taarifa zilizothibitishwa zinadai kuwa nyumba hiyo ambayo kijana huyo amepigwa shoto ilikuwa na tatizo la umeme ambalo lilitolewa taarifa kwenye shirika la Umeme TANESCO mkoa wa Morogoro lakini tatizo hilo lilishindwa kutatulia na TANESCO mpaka leo ambapo shoti hiyo imesababisha kifo cha kijana huyo.
Baada ya kutoa kifo cha kijana huyo kabla ya mwili wake kuondolewa ndipo mafundi wa TANESCO walipofika na kuzima umeme kwa ajili ya kuanza uchunguzi wa tatizo hilo chini ya ulinzi wa jeshi la polisi kwa kuhofia wananchi kuchukua sheria mkononi dhidi ya mafundi hao wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

No comments:
Post a Comment