Wednesday, January 3, 2018

Elimu bure bado changamoto mkoani Mtwara

Walimu wa shule ya msingi Mbae yenye wanafunzi 513  iliyopo Manispaa ya Mtwara Mikindani wanalazimika kutumia vivuli ya miti ya mikorosho kama ofisi hali inayoathiri utendaji wao wa kazi hasa kipindi hiki  cha mvua.

Akizungumza  na waandishi wa habari Mkuu wa shule ya msingi Mbae Gerard Musa amesema shule hiyo ilianzishwa mwaka 2015 inamadarasa matatu huku ikiwa haina ofisi za  walimu hali inayopelekea kufanya kazi katika mazingira magumu.

Kufuatia hali hiyo ameomba wafadhili mbalimbali kujiteokeza ili kusaidia ujenzi wa ofisi za walimu pamoja na madarasa ili kuiwezesha manispaa kutatua changamoto hiyo ambayo ni kikwazo kwa wanafunzi wa shule hiyo.

Kwa upande wake Afisa Elimu wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Flora Alois amesema Manispaa inatambua changamoto za shule hiyo na tayari imetenga bajeti kwa mwaka 2017-2018  ili kujenga ofisi ya walimu sambamba na madarasa mawili.

Hata hivyo amesema Manispaa kwa kushirikiana na wafadhili imefanikiwa kupunguza baadhi ya changamoto katika shule hiyo ikiwemo kujenga matundu kumi ya vyoo.

No comments: