Naibu Waziri wa Afya ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi mkoani Kigoma ambapo amesema kwa sasa upatikanaji wa dawa ni wa uhakika hivyo hakuna sababu ya wagonjwa kukosa dawa katika vituo vya kutolea huduma za afya.
Kwa upande wao wananchi wa kijiji cha Nyakitonto wilaya ya Kasulu wameishukuru serikali kutoa shilingi milioni 700 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya na vifaa tiba na kwamba ujenzi huo utasaidia kuondokana na changamoto ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma ya afya katika maeneo mengine.

No comments:
Post a Comment