Monday, January 22, 2018

Waziri Jaffo atoa agizo kwa watendaji wa manispaa


Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa TAMISEMI, Suleiman Jaffo amewaagiza watendaji wa manispaa zinazotekeleza miradi ya uboreshaji wa miundombinu katika jiji la Dar es Salaam DMDP kuhakikisha wanawasimamia wakandarasi waliopewa zabuni ya utekelezaji wa miradi hiyo katika kiwango cha ubora na endapo watabaini kuwa hafanyi vizuri wamuondoe mapema ili kuepuka hasara inayoweza kutokea.

Ametoa maagizo hayo jijini humo alipotembelea baadhi ya miradi inayotekelezwa katika manispaa ya Ilala na kinondoni ambapo ziara yake ilianzia katika barabara ya buguruni kwa mnayamani manispaa ya Ilala ambako awali aliagiza kufanyiwa marekebisho ya mabomba ya maji yaliyokuwa yakimwagika barabarani na kuingia kwenye majumba na kukuta eneo hilo limekaa vizuri lakini aliagiza kujengwa barabara hiyo kwa kiwango cha lami katika muda mfupi kwa kuzingatia viwango vya ubora ili iweze kudumu kwa muda mrefu huku wakizingatia giografia ya eneo husika.

Akiwa katika barabara ya Makumbusho manispaa ya kinondoni inayojengwa kwa kiwango cha lami amesema atashangaa kuona barabara hizo zenye garantii ya miaka 20 zinaharibika ndani ya muda mfupi kwani gharama zinazotumika ni kubwa ikilinganishwa na mradi wa miji nane huku akisistiza kuwa miradi hii ya DMDP inasimamiwa na kuleta matokeo chanya.

No comments: