Thursday, June 21, 2018

Muhimbili sasa kufanya operesheni ya tumbo bila kupasua


Madaktari bingwa wa magonjwa ya mfumo wa chakula na ini kutoka hospitali ya Taifa Muhimbili wamefanikiwa kufanya oparesheni ya viungo hivyo pasipo kuhusisha upasuaji wa kifua wala tumbo.

Wakiongea na wataalamu wa mfumo wa chakula kutoka nchi zilizoendelea duniani Daktari bingwa wa magonjwa hayo Dkt.John Rwegasha amesema utaalamu waliopata kwa kushirikiana na wataalamu kutoka nchini India ambapo kwa nchi za Afrika Mashariki ni nchi ya kwanza kufanya oparesheni huo.

Nao baadhi ya wataalamu kutoka nchini India wamesema ni jambo jema kushirikiana na nchi zilizoendelea kiteknolojia hasa ya matibabu ili kuokoa maisha ya watanzania hasa wale wenye kipato cha chini ambao hawawezi kwenda nje ya nchi kwa matibabu.

Aidha, Jopo la madaktari hao wamesema kupitia mafunzo mbalimbali waliyoyapata nchini India miezi kadhaa iliyopita na hivyo wamerudi wakiwa wamebobea na utaalam huo wa kufanya oparesheni Kwa kutumia Kifaa cha Hadubini katika kufanya oparesheni za kongosho na ini.

No comments: