RAIS mstaafu Benjamini Mkapa kesho Agosti 08, atakuwa Mgen Rasmi katika Kilele cha Maonesho ya Sherehe ya wakulima Nanenane Kitaifa mwaka 2018, ambayo yanafanyika katika Uwanja wa Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Akizungumza na vyombo vya habari , Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka amesema Mkapa atakuwa mgeni rasmi katika madhimisho hayo akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Amesema pia katika kilele cha Maadhimisho ya maonesho hayo viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali watashiriki wakiwemo Katibu Mkuu wa CCM , Dkt. Bashiru Ally Sambamba na Mawaziri, Manaibu Waziri na Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Mkuu wa wizara mbalimbali.
“Watakuwepo viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali pamoja na viongozi wa Taasisi mbalimbali za Fedha wakiwemo Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania(BOT) Prof. Florens Luoga na Mkurugenzi wa Benki ya NBC, Theobald Sabi”
No comments:
Post a Comment