
Rais Donald Trump wa Marekani amekutana na mweziye wa Kenya Uhuru Kenyatta mjini Washington na uzungumzia masuala mbalimbali.
Hata hivyo mazungumzo yao yaligubikwa na msiba wa aliyekuwa mgombea wa Urais wa Marekani na Seneta wa muda mrefu katika bunge la nchi hiyo John McCain.
Rais Kenyatta ni kiongozi wa pili kutoka kusini mwa Jangwa la Sahara kukaribisha Ikulu ya White House na kufanya mazungumzo na Rais Trump.

Viongozi hao wawili kwa pamoja wamejadili njia za pamoja za kupambana na ugaidi na ushirikiano wa kibiashara.
Mpango wa upanuzi wa barabara inayohusisha miji mikubwa ya Kenya, Mombasa na Nairobi pia ilijadiliwa.
Kwa upande wake Rais Uhuru Kenyatta ameandika katika mtandao wa Tweeter kwamba amefanikisha makubaliano yenye thamani ya mamilioni ya dola na Wawekezaji wa Kimarekani.
Katika siku za hivi karibuni China imeipita Marekani kwa kuwa na uwekezaji mkubwa nchini Kenya.
Hata hivyo Rais Kenyatta ameonekana kuwa na bidii ya kuwakubali washirika wote kibiashara.
Baadaye wiki hii pia anatarajia kumpokea jijini Nairobi, Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May, kabla ya kufunga safari kuelekea Beijing, kwenye mkutano wa pamoja wa Afrika na China.
No comments:
Post a Comment