Monday, September 3, 2018

Polisi Arusha yafunguka juu ya ajali iliyoua watu sita wakiwemo watalii


Jeshi la polisi  mkoani Arusha limetoa maelezo ya awali ya chanzo cha ajali mbaya iliyotokea eneo la mti mmoja  wilayani  Monduli na kusababisha vifo vya watu sita wakiwemo raia watatu wa kigeni na wengine watatu kujeruhiwa.

Akizungumza  ajali  hiyo kamanda wa polisi wa mkoa wa Arusha Ramadhani Nga’nzi  pamoja  na kutoa taarifa hiyo pia  amesema  taratibu  za  kuwatambua  marehemu   na  nchi   wanakotoka zinaendelea.

Majeruhi  walionusurika kweye  ajali  hiyo  ambao wamelazwa kwenye  hospitali  ya  mkoa  wa  Arusha ya Mount  Meru  na  wengine  hospitali ya Lutheran  ya Arusha  ambao  walikuwa kwenye lori wamesema  gari  lao  lilipata hitilafu  kwenye  mfumo  wa  breki.

Kaimu mganga  mkuu wa hospitali ya mkoa wa Arusha ya Mount  Meru Dkt. Othumani  Chande  na  Dkt. Peter  Mabula  wa  hospitali  ya Arusha  Luthrani   wamethibitisha  kupokea  miili  mitano  ya marehemu waliofariki katika eneo la ajali na kwamba  mmoja alifariki  wakati  wanapatiwa matibabu.

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ametembelea  majeruhi  na kwamba  taratibu juu ya raia  wa  kigeni waliofariki  zinaendelea .

No comments: