AJALI YA MBALIZI MBEYA ILIYO UA WATU KUMI NA MOJA |
Na: Mwandishi wetu
ILE
ajali ya kutisha iliyoshirikisha magari matatu, likiwemo la Mbunge wa
Viti Maalum kwa tiketi ya CCM, Mkoa wa Mbeya, Dk. Marry Mwanjelwa na
kuua watu 11, imesimuliwa mambo ya kutisha, Risasi Jumamosi linashuka
nayo.
Tukio
hilo lilitokea Oktoba 2, mwaka huu, Mbalizi, Mbeya Vijijini ambapo
magari matatu, likiwemo lori lililosababisha ajali yaligongana na
kupinduka kisha kuwaka moto na kuteketea na baadhi ya watu.
Kwa
mujibu wa mashuhuda waliozungumza na Risasi Jumamosi, hakuna shaka eneo
hilo limetawaliwa na majini kwa vile haupiti mwezi bila kutokea ajali
ya kutisha.
“Sisi
tunasema hapa kuna majini jamani, hapapiti mwezi lazima itokee ajali,
serikali ielewe hilo jamani,” alisema Mzee Simon Mwalusale, mkazi wa ene
hilo.
Pia yapo maelezo kuwa, mapema siku ya tukio, kulionekana noti za shilingi elfu kumi zikipeperuka eneo hilo na watu waliziokota.
“Kuna
jambo lingine la ajabu sana, siku ya tukio, mapema zilionekana noti za
elfu kumikumi, watu waliziokota licha ya kwamba hazikujulikana
zilikokuwa zikitokea.
“Cha
kushangaza, zile noti zilikuwa na damudamu, lakini hilo watu
hawakulijali, waliziokota na kuziweka mifukoni mwao,” aliongeza mzee
huyo.
Wakati
huohuo, umoja wa wachungaji, Mbalizi, wakiongozwa na mchungaji
aliyetambulika kwa jina moja la Daudi wanajipanga kufanya maombi eneo
hilo ili kama kuna nguvu za giza zinazosababisha ajali mara kwa mara
ziondoke.
Oktoba
4, 2012, jijini Dar katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili, Dk. Mwanjelwa
ambaye alifikishwa hospitalini hapo kutoka Mbeya kwa matibabu zaidi,
alizungumza na mwandishi wetu akiwa katika chumba maalum cha uangalizi.
“Nilikuwa
nikishuhudia ile ajali kwani lori lilikuwa nyuma yetu kwa kasi huku
likionekana breki ziligoma na ndipo lilipotuvamia na kutugonga.
“Nilisikia kishindo kikubwa kikitokea, nilijua ndiyo mwisho wa uhai wangu hapa duniani, lakini Mungu mkubwa bado niko hai.
“Nawashukuru
wasamaria wema na askari waliokuja kutuokoa, ila nimeumia sana
niliposikia kuna watu 11 walikufa na wengine kujeruhiwa vibaya.
“Sasa
naendelea vizuri tofauti na nilivyoletwa (Jumatano), nawashukuru
madaktari na wauguzi kwa jitihada zao,” alisema Dk. Mwanjelwa.
CHANZO: GLOBAL PUBLISHERS INFO
DR MARY MWANJELWA MBUNGE VITI MAALUM MBEYA |
Akiwa katika matibabu Dar es salam kwa mbeya uchaguzi ulikuwa unaendelea na Mary Mwanjelwa akiwaMjumbe wa Baraza Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM mkoa, aliyekuwa
akitetea nafasi hiyo Dk.Mary alijikuta akishindwa vibaya na mpinzani wake
mkubwa kisiasa, Edina Mwaigomole.
Dk.Mary na Edina ni wanasiasa wanaokubalika ndani ya UWT mkoani
hapa na wenye upinzani mkali kisiasa, kwani hata katika kinyang’anyiro cha
ubunge viti maalum mkoani hapa walishindana kwa kura chache.
Nafasi ya ujumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa, ambayo ilikuwa na
wagombea watatu, Shizya Mwakatundu, ambaye pia ni Mwenyekiti wa UWT wilaya ya
Mbeya mjini ameibuka kidedea.
No comments:
Post a Comment