BARABARA YA ILEJE NA CHANGAMOTO ZAKE KESHO KUTWA NASAFIRI KWENDA HUKO NGOJA TUKAJIONEE KULIVYO TUWE SOTE KATIKA SAFARI |
UBOVU
wa bara bara katika Wilaya ya Ileje Mkoani Mbeya umesababisha hali za
maisha za wananchi wa wilaya hiyo kuendelea kuwa duni kutokana na
kushindwa kusafilisha mazao wanayolima kwenda mikoa mingine.
Akizungumza na mwandishi Esthar Macha mdau wa mtandao
huu ofisini kwake Mkuu wa Wilaya ya Ileje Bi.Rosemary Senyamule
alisema hayo kufuatia ubovu huo wa bara bara ambao umedumu kwa muda
mrefu bila jitihada zozote za kuhakikisha kuwa zinatengenezwa ili
wananchi waweze kuwa na hali nzuri za kimaisha.
Alisema
kuwa ubovu huo wa bara bara umekuwa ni tatizo kubwa kwa wananchi na
hata kushindwa kushindwa kusafilisha mazao na vitu vingine ambavyo ni
mkombozi kwa wananchi ambavyo vingeweza kuokoa hali za maisha.
“Hili
suala la miundo mbinu katika wilaya hii ni tatizo kubwa sana ambalo
linasababisha uchumi wa wananchi wa wilaya hii kuendelea duni ,ili
kuweza kufanikisha hili serikali inaendelea kufanya jitihada ili
kuhakikisha kuwa miundo mbinu hii inatengenezwa mapema”alisema.
Mkuu
huyo wa Wilaya alisema hilo likifanikisha hali ya uchumi kwa wananchi
itaweza kubadilika haraka na wanancghi kuweza kufanya kazi zao kwa mara
moja ,hivi sasa safari ya kutoka Mpemba Ileje mwananchi anatumia masaa
matatu mpaka manne wakati ni safari ya saa moja tu.
Aidha
Bi.Senyamule alisema kama serikali wanaendelea na na jitihada aza
kuhakikisha kuwa bara bara hiyo inatengenezwa na kupewa kipaumbele
kwenye bajeti ijayo .
Mmoja
wa wananchi wa Tarafa ya Kipambawe Wilayani hapa Bw.Sifanuel Luka
alisema kuwa tatizo la kutokuwa na bara bara nzuri katika wilaya hiyo
limekuwa ni shida kubwa kwao kwa kushindwa kusafirisha vitu muhimu kwao
ambavyo vingeweza kuondoa ugumu wa maisha.
“Kwa
ujumla hili ni tatizo kubwa sana sehemu ya kwenda na kurudi inakulazimu
mpaka ulale kwa hali hii maisha lazima yawe magumu kwa sisi
wananchi,wilaya hii ni muda mrefu hebu angalia maisha ya wananchi wa
wilaya hii walivyo na maisha magumu serikali ifanye jitihada mapema
kuhakikisha kuwa bara bara hii inatengenezwa haraka”alisema.
o752-881456
Kingo
No comments:
Post a Comment