DNA Yabaini Watoto Wengi Wa Kusingiziwa
Na Florence Majani, MWANANCHI
ASILIMIA 44 ya wapenzi wanaokwenda Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali
kupima vinasaba (DNA), kwa ajili ya kujua uhalali wa watoto kwa baba,
wamethibitishiwa kuwa watoto hao si wa kwao.
Takwimu za mwaka 2012 kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali,
zimeainisha kuwa kati ya watu 90 waliokwenda kupima DNA, 40 ambao ni sawa na
asilimia 44, wameonekana kubambikiziwa watoto.
Takwimu hizo za kuanzia Januari hadi Oktoba mwaka huu, zilionyesha kuwa
katika kesi 50 za waliokwenda kupima, matokeo yalionyesha kuwa ni wazazi halisi
wa watoto wao.
Hata hivyo, idadi hiyo inayoonyesha kuwa kinababa siyo wazazi halisi wa
watoto, imeshuka ikilinganishwa na takwimu za mwaka 2008/2009 ambazo
zinaonyesha kuwa asilimia 60 ya watu waliochukua vipimo hivyo wamebainika kuwa
si wazazi halisi wa watoto hao.
Wakati huohuo
Ujue utamaduni wa kabila la wasafwa wa jijini Mbeya
na
Mkazi
wa Mwasanga jijini Mbeya Sosteli Mponzi (kulia) akimuonyesha Victoria
Zitta Mnyanyi (kushoto) ambaye ni Mshauri wa wanafunzi wa chuo kikuu cha
Mzumbe tawi la Mbeya moja ya nyumba ya kale iliyokuwa inatumiwa na
kabila la wasafwa ambalo ni kabila maarufu mkoani humo. Mponzi ameamua
kujitolea kujenga kituo cha utamaduni wa kabila hilo ambacho kitatunza
kumbukumbu za utamaduni na mila zote ili kizazi kijacho kiweze kufahamu
mambo yaliyofanywa na mababu zao.
Msafwa
wa Mwasanga jijini Mbeya Ibrahim Saimon akipuliza pembe ya Mnyama aina
ya Tandala “Ndundwe” iliyokuwa inapingwa wakati wa sherehe za kumaliza
msiba “matanga” za kabila la wasafwa. Sosteli Mponzi ameamua kujitolea
kujenga kituo cha kutunza utamaduni na mila za kabila hilo ili kizazi
kijacho kiweze kufahamu mambo yaliyofanywa na mababu zao.
Baadhi
ya wasafwa wa Mwasanga jijini Mbeya wakimuangalia Mary John akisaga
unga wa ulezi kwa kutumia jiwe aina ya “Lwala” wakati walipotembelea ili
kujionea ujenzi wa kituo cha utamaduni wa kabila lao kinachojengwa kwa
kujitolea na Sosteli Mponzi. Baadhi ya wasafwa waishio maeneo ya
vijijini bado wanasaga unga wa ulezi kwa kutumia jiwe hilo kwa ajili ya
kutengenezea pombe.
Mkazi
wa Mwasanga jijini Mbeya Sosteli Mponzi (kushoto) akimuonyesha Victoria
Zitta Mnyanyi ambaye ni mshauri wa wanafunzi wa chuo kikuu cha Mzumbe
tawi la Mbeya mti wa asili aina ya msulusulu ambao wazee wa kabila la
wasafwa walikuwa wakiutumia kwa ajili ya kutibu mifugo. Mponzi ameamua
kujitolea kujenga kituo cha utamaduni wa kabila hilo ili kumbukumbu
zisiweze kupotea kwani hivi sasa kutokana na utandawazi makabila mengi
yamekuwa yakipoteza utamaduni wao.
Baadhi
ya wasafwa wa Mwasanga jijini Mbeya wakicheza ngoma aina ya Mbeta ya
kabila hilo ambayo inachezwa wakati wa kumaliza msiba “Mwengulo” kama
walivyokutwa na mpiga picha wetu hivi karibuni alipotembelea kituo cha
kutunza utamaduni na mila za kabila la wasafwa. Ujenzi wa kituo hicho
unajengwa kwa kujitolea na Sosteli Mponzi ili kizazi kijacho kiweze
kufahamu mambo yaliyofanywa na mababu zao.
Mkazi
wa Mwasanga jijini Mbeya Juma Changa akionyesha jinsi wazee wa zamani
walivyokuwa wakichonga mpini wa jembe kwa kutuma teso “menzo” wakati
mpiga picha wetu alipotembelea kituo cha kutunza utamaduni na mila za
kabila la wasafwa huku Said Mbata (kulia), Victoria Zitta Mnyanyi
(katikatia) na Sosteli Mponzi (kushoto) wakimuangalia. Ujenzi wa kituo
hicho unajengwa kwa kujitolea na Mponzi ili kizazi kijacho kiweze
kufahamu mambo yaliyofanywa na mababu zao.
Baadhi
ya wasafwa wa Mwasanga jijini Mbeya wakimwonyesha mpiga picha wetu
jinsi wazee wa zamani wa kabila hilo walivyokuwa wanakunywa pombe aina
ya Kimpumu wakati alipotembelea kujionea ujenzi wa kituo cha kutunza
utamaduni na mila za kabila hilo.Kutokana na kuenea kwa magonjwa
mbalimbali ya kuambukiza hivi sasa kila mtu anakunywa pombe hiyo kwa
kutumia chombo chake.
na
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA (TCRA) YATOA ZAIDI YA SHILINGI MILION 15 KWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA AJILI YA KUBORESHA MFUMO MPYA WA UTOAJI HUDUMA ZA MATIBABU KWA NJIA YA MAWASILIANO (TELE MEDICINE)
ZAIDI ya shilingi million
15 zimetolewa na mamlaka ya mawasiliano Tanzanzania (TCRA) nyanda za juu
kusini ajiri ya kuboresha mfumo mpya wa utoaji
huduma za matibabu kwa njia ya mawasiliano (TELE MEDICINE) ili kupunguza
vifo na gharama za usafiri kwa wagonjwa.
Jengo la TTCL Mbeya |
Mitambo ya kisasa ya mkonge wa taifa |
![]() |
Hudi iliyokabidhiwa leo |
Moja ya wataalam wa mkonge wa taifa Humphrey Ngowi akiwaeleza waandishi wa habari jinsi mtambo huo unavyofanya kazi |
WANANCHI SONGWE MBEYA WAANDAMANA KUTAKA MATUTA
![]() |
SISI NI WANAFUNZI, WAZAZI NA WENZETU WAMEPOTEZA MAISHA
HAPA KWA KUGONGWA INGAWA KUNA PUNDA MILIA LAKINI MADEREVA HAWAJALI KAULI ILE YA
KIBURI SI MAUNGWANA
|
![]() |
JAMANI SISI NI VIONGOZI WA WILAYA HII, TUNAOMBA
MTUSIKILIZE
|
![]() |
NAITWA SIMON MKINA KAIMU MENEJA
WA TANROAD MBEYA, KWA LEO HAIWEZEKANI LAKINI TUTAJENGA MATUTA
|
No comments:
Post a Comment