Waziri Aingilia Mgogoro Kati Ya Kiwanda Na Wananchi
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka (kulia) akiongea na Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha Saruji cha Twiga (Twiga Cement) Bw.Pascal Lessoinne (kushoto) mara baada ya mkurugenzi huyo kutoa taarifa fupi ya maendeleo ya kiwanda hicho na hali ya mvutano wa muda mrefu wa umiliki wa maeneo baina ya wakazi wa kata za Bunju na Wazo jijini Dar es salaam.
Picha
na 2. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna
Tibaijuka akiwasalimia wakazi wa kata ya Bunju na Wazo mara baada ya
kuwasili katika eneo hilo kwa lengo la kuzungumza nao ili kutafuta suluhisho la kudumu la mgogoro wa ardhi kati yao na kiwanda cha Saruji cha Twiga jana jioni.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka akiongea katika mkutano wa hadhara na maelfu ya wakazi wa kata ya Wazo na Bunju waliojitokeza kufuatilia maendeleo ya mgogoro wa ardhi kati yao na Kiwanda cha Twiga Cement ambapo pamoja na mambo mengine amewahakikishia wakazi hao kuwa mgogoro huo utapatiwa ufumbuzi wa kudumu na kuwaomba kutoa ushirikiano kwake.
Diwani wa eneo la Bunju na Wazo Sharif Exavery Majisafi akiongea na wananchi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka kuzungumza nao.
Sehemu ya umati mkubwa wa wakazi wa kata za Bunju na Wazo
wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Prof. Anna Tibaijuka.
.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO DSM
NA

Mtumishi
wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Gladness Mangelele akitoa maelezo
mbele ya Waziri Dk. Mwakyembe baada ya kuhusishwa katika sakata hilo
ambapo alidai alikuwa hajui chochote kwani alikuwa akitekeleza majukumu
yake ya kawaida katika idara yake.

Dk.
Mwakyembe akikagua Malori yanayodaiwa kutaka kutolewa kinyemela na
kampuni ya Dhandho, Malori matano kati ya 26 yalipewa baraka na Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) yatolewe.

Marystella Minja akitoa maelezo yake mbele ya Waziri Dk Harrison Mwakyembe baada ya kutuhumiwa katika sakata hilo.

Mmoja
wa wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari (TPA) Andrew Masaga (kulia)
anayedaiwa kuhusika kula njama ya kutoa malori hayo akijitetea mbele ya
Waziri (hayupo pichani) katika sakata hilo jana jinoni. Kushoto ni Mkuu
wa Polisi Bandarini Afande FM Misilimu

Ofisa Utawala wa kampuni ya Dhandho Antipasi Otieno (kulia) akitoa maelezo mbele ya waziri Dk. Harrison Mwakyembe

Waziri
wa Uchukuzi Dk. Harisson Mwakyembe akizungumza na waadishi wa habari
Bandarini jijini Dar es salaam Jana jioni wakati akitoa taarifa ya
kukamatwa kwa watumishi wa Bandari wanaodaiwa kutaka kutoa malori 26
kinyemela bandarini, watu watano wamekamatwa katika sakata hilo.

Dk.
Harrison Mwakyembe akiongea na maafisa mbalimbali wa Polisi na Bandari
baada ya kukagua magari hayo yaliyotaka kutolewa kinyemela bandarini
hapo
PIA

KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Bw. Nape Nnauye
--
Na Mwandishi Wetu-Gazeti la Majira
KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Nape Nnauye, amempongeza Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kwa kukiri kumiliki kadi ya chama chao hadi sasa.
Alisema Dkt. Slaa ameanza kujifunza kusema ukweli baada ya kutambua uongo haulipi kwani kitendo cha kukiri kumiliki kadi ya CCM ni cha kiungwana hivyo anastahili pongezi.
Bw. Nnauye aliyasema hayo Dar es Salaam jana baada ya Dkt. Slaa kujibu tuhuma zake kuwa, wapo baadhi ya vigogo wa CHADEMA ambao wanamiliki kadi za CCM na wanazilipia hadi sasa.
“Dkt. Slaa amekiri katika vyombo vya habari kuwa anamiliki kadi ya CCM hadi sasa akidai anaitunza kama kumbukumbu muhimu hivyo ni vyema akawaeleza Watanzania kadi yake ameilipia hadi lini na aache kuwadanganya wenzake warudishe kadi za chama tawala wakati yeye ameendelea kuwa nayo,” alisema.
Bw. Nnauye amekiri kumheshimu sana Dkt. Slaa kama babu yake na alishtuka sana kusikia Katibu Mkuu huyo anawatuhumu baadhi ya viongozi wa CHADEMA na kudai ni mamluki wa CCM wakati yeye ni namba moja kwani anaowatuhumu hawana kadi za chama hicho.
“Nilimsikia Dkt. Slaa akiwatuhumu baadhi ya viongozi ndani ya chama chao kuwa ni mamluki wa CCM, hili linawasaidiaje Watanzania maskini.
“Kitendo hiki kimethibitisha upeo mdogo alionao katika kufikiri, huyu ni kiongozi mkubwa ambaye namuheshimu lakini anapaswa kujua yeye anaomba kuwa kiongozi hivyo lazima wananchi tumjue tabia zake,” alisema Bw. Nnauye na kuongeza;
“Viongozi wa aina yake ni janga kwa Taifa letu, usipokuwa mwaminifu kwa kidogo, huwezi kuwa mwaminifu kwa kikubwa,” alisema.

Kipanya Leo NA DNA

TUMSAIDIE MTANZANIA MWENZETU
Bi Arafa akiwa na Msamaria mwema anaemsaidia kuhakikisha hali ya Mgonjwa huyo Inaimarika.
Bi Arafa Issa akiwa katika kitanda cha ward namba 20 Sewa Haji-Muhimbili hosp asubuhi ya leo.
--
Bi Arafa
Issa mwenye umri wa Miaka 38 mkazi wa Kijiji cha Narung'ombe wilayani
Ruangwa ambae anasumbuliwa na Uvimbe baada ya kuumwa Kichwa na baadae
kupata kipele kilichosababisha Uvimbe kama anavyoonekana Pichani,
alifikishwa katika Hospital ya Muhimbili baada ya Wasamaria wema
walioguswa na hali hiyo pamoja na Ofisi ya Mkurugenzi mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi kujitoa kumsaidia
kumsafirisha toka Kijijini kwao hadi Muhimbili Hospital.
Baada ya
kufikishwa na kupokelewa amelazwa Block la Sewa Haji Ward na 20 NA
Baadae alitakiwa kupimwa kipimo cha CT Scan kufuatia kipimo hicho
Wauguzi wake waliambiwa kipimo hicho kina tatizo na kuelekezwa kwenda
Regency Hospital kupima hali iliyokuwa ngumu kwao kutokana na gharama
kubwa kwao ya kumudu kipimo hicho Tshs(264,000/-).
Kwa msaada mwingine Wadau walifanikisha kupimwa kwa mgonjwa huyo na kupatiwa majibu ambayo yanaelekeza kufanyiwa Upasuaji..
Asubuhi
ya Leo nilifika katika hospital hiyo na kuonana na Bi Arafa ambae
analalamika sana kupata maumizi makubwa Kichwa na kudai kuwa toka
amepokewa katika hospital hiyo na kulazwa tarehe 20 NOV 2012 hadi leo
ajapata dawa ya aina yoyote zaidi ya panadol anazonunua hali inapomzidi.
Nilifanikiwa
kuwasiliana na muuguzi aliekuwepo zamu asb na baada ya kupitia file
lake alinikabidhi fomu inayoonyesha mgonjwa anatakiwa apime kipimo
kinaitwa MRI Brains na kuelekeza sehemu ya kwenda kulipia kipimo
hicho...Baada ya kuwasilisha hiyo fomu imetakiwa Tshs Laki
mbili(200,000)Pia itahitajika gharama ya Operesheni ambayo haikutajwa.
Kwa niaba
ya Bi Arafa Nawaomba wadau mbalimbali ndugu na jamaa kusaidia hatua
inayofuata kumsadia mgonjwa huyo..Yupo hapo Hospital Unaweza kusaidia
kwa njia moja au nyingine.
Kwa
Mawasiliano zaidi ya mgonjwa huyo wasiliana nami kwa 0716
483532,0787176221 au 0716483532 Abdulaziz Ahmeid wa Lindi Press Club
au abdulaziz762@gmail.com
Nawashukuru wote walioguswa kumsaidia Mgonjwa huyo hadi ilipofikia leo,,Ameen
BURUDANI

Washiriki
wa shindano la Miss East Afrika 2012 wakiwa katika picha ya pamoja
mapema leo mchana
jijini Dar.
No comments:
Post a Comment