SIKU TULIPOANDAMANA WAANDISHI WA HABARI MBEYA KUPINGA MAUAJI YA KIKATILI YALIYOFANYWA N JESHI LA POLISI MKOA WA IRINGA KWA MWANDISHI DAUDI MWANGOSI |
SIKU YA MAANDAMANO YA AMANI KWA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA MBEYA |
BAADHI YA WAANDISHI WA MKOA WA MBEYA |
KATIBU WA CHADEMA DR SILAA AKITOA SALAM ZA RAMBIRAMBI SIKU YA MAZIKO YA DAUDI MWANGOSI |
PROF MACK MWANDOSYA MBUNGE WA RUNGWE MASHARIKI AKITOA RAMBIRAMBI SIKU YA MAZIKO YA DAUDI MWANGOSI KIJIJI KWAO BUSOKA WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA |
WAWAKILISHI WA CHANNELTEN WAKIWA PEMBENI YA KABURI LA MWENZAO DAUDI MWANGOSI |
![]() |
MAREHEMU DAUD MWANGOSI ENZI ZA UHAI WAKE . BADO MACHUNGU HAYAJAFUTIKA POLISI HAOHAO TENA WAMPIGA RISASI MWANDISHI WA HABARI SHABANI MATUTU. |
Mwandishi Aliyepigwa Risasi Anaendelea Na Matibabu MOI
Ukistaajabu Ya Mussa Utayaona Ya Firauni
Katika pitapita zake kwenye manispaa ya Moshi , kamera ya ikanasa tukio hili huyu ni binti wa miaka 14 na tayari ana watoto wawili
MICHEZO
NGASSA ATUA MERREIKH KWA DOLA 75,000 NA MSHAHARA MNONO WA DOLA 4,000 YEYE MWENYEWE AKATIWA DOLA 50,000 ZA WINO
![]() |
Ngssa; Sasa mutu ya fweza |
Na Mahmoud Zubeiry,
Kampala
BIASHARA
imeisha. Azam FC imemuuza Mrisho Khalfan Ngassa kwa dola za Kimarekani 75,000
kwenda El Merreikh ya Sudan ambako amesaini mkataba wa miaka miwili,
utakaomuwezesha kulipwa mshahara wa dola za Kimarekani 4,000 kwa mwezi huku naye
akilipwa dola 50,000 za kusaini.
Awali,
Merreikh walitaka kumpa mkataba wa miaka mitatu Ngassa wenye thamani ya dola
100,000, lakini wakala wake Alhaj Yussuf Said Bakhresa akakataa akisema
utambana mchezaji wake aking’ara na kutakiwa na klabu nyingine.
Sasa Ngassa
baada ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge mwishoni
mwa wiki hii, atakwenda Sudan kufanyiwa vipimo tayari kujiunga na klabu hiyo, ambayo
ni jambo la kawaida kucheza hatua ya makundi ya michuano ya klabu Afrika.
Azam FC
imesema imeweka mbele maslahi ya mchezaji na taifa kwa ujumla katika maamuzi ya
kumuuza Sudan, kutoka Simba alikokuwa akicheza kwa mkopo. “Hii timu (Merreikh)
kila mwaka inacheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, maana yake
huyu mchezaji atakwenda kupata maendeleo na kuja kuisaidia zaidi Tanzania
katika mashindano ya kimataifa,”alisema kiongozi mmoja wa Azam.
Alipoulizwa kuhusu
Simba SC aliyokuwa anaichezea klabu hiyo, kiongozi huyo alisema wao walimtoa
kwa mkopo Ngassa kwenda kwa Wekundu wa Msimbazi hadi Mei 31, mwakani na mkataba
wao ndio unasema hivyo.
“Sisi
tuliwapa Simba huyu mchezaji kwa mkopo hadi Mei 31 na wakatupa Sh. Milioni 25,
ila tuko tayari kuwarudishia fedha zao walizota, lakini huyu mchezaji ni mali
yetu na hata TFF wanatambua hilo, na
tumekwishamuuza Merreikh,”alisema.
Alipoulizwa kuhusu
Simba kusaini mkataba mpya na Ngassa, alisema; “We uliona wapi dunia nzima timu
inapewa mchezaji kwa mkopo halafu inamsainisha mkataba? Simba lazima ifike
wakati waache kurudia makosa, haya ndio mambo ya Mbuyu Twite sasa,”alisema
kiongozi huyo wa Azam.
Katika kukamilisha
mauzo ya mchezaji huyo, kiongozi wa Marreikh akiwa Dar es Salaam mbele ya
viongozi wa TFF na Azam, alipigiwa simu Ngassa aliye hapa Kampala, Uganda na
kuhusishwa katika dili hilo, naye akakubali ndipo mambo yakamalizwa.
Aidha, Azam wameomba
TFF ihakikishe kunakuwa na ulinzi katika kambi ya timu ya taifa mjini hapa, ili
Simba wasimfanyie vurugu Ngassa na kumvuruga kisaIkolojia, wakati ndiyE tegemeo
la timu katika kampeni ya kutwaa Kombe la Challenge mwaka huu mjiini hapa.
Kwa upande
wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe
akizungumza kutoka Dar es Salaam, alisema kwamba watawapeleka mahakamani Azam kwa
kitendo cha kumuuza mchezaji wao kinyume cha sheria.
“Haiwezekani
wamuuze wao, wakati wao walituuzia huyu mchezaji na sisi tuna mkataba ambao
tulisaini nao, hii ni kinyume cha sheria na sisi tutawapeleka mahakamani,”alisema
Hans Poppe ambaye anatua kesho mjini hapa.
Azam
walimtoa kwa mkopo Ngassa mwanzoni mwa Agosti, mwaka huu baada ya kukerwa na
kitendo cha mchezaji huyo kubusu jezi ya timu yake ya zamani, Yanga, katika
Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, dhidi
ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Alifanya
hivyo, baada ya kufunga bao la ushindi akitokea benchi na kuiwezesha Azam
kutinga fainali ya michuano hiyo, ambako walifungwa na Yanga 2-0, naye kwa mara
nyingine akitokea benchi na kushindwa kufunga, hivyo kutuhumiwa kucheza kinazi.
Ilielezwa
kwamba Simba walitoa Sh. Milioni 25 kumnunua kwa mkopo mchezaji huyo, ingawa
baadaye Simba wakasema waliununua mkataba wa mwaka mmoja aliobakiza mchezaji
huyo Azam FC, nao wakamuongezea wa mwaka mmoja kwa kumsainisha kwa Sh. Milioni
30, kati ya hizo Milioni 12 akipewa taslimu na 18 akipewa gari.BURUDANI
UKITAKA KUOA SIKU HIZI LAZIMA UJIPANGE SAWASAWA LASIVYO UTAUMBUKA |
mhh ndio maana wanaume wanaogopa kuoa ( wapo wapo saaaaaaana!!!!!!jamani embu cheki hii ..... Hivi jamani, mnazijua gharama anazoingia bwana harusi hadi anapooa? Katika hali ya kawaida kabisa, kama wewe ni mwanaume na unataka kuoa, jiandae kwa mambo haya:
1. Kujitambulisha ukweni. Hapo utatakiwa uende kijijini alikozaliwa mkeo mtarajiwa ukajitambulishe huko. Kama mfano
mkeo
anatokea Mwanza, na mnaishi Dar, andaa nauli ya watu wawili, malazi kwa
siku mbili, na utagharamia shuhuli hiyo ya utambulisho. We tenga
500,000. Hapo tuna assume mkeo atajitegemea. Otherwise 800,000
itakutoka.
2. Kumtambulisha mkeo kwenu. Kama nyie nyumbani ni Arusha, utatakiwa umpeleke huko Ngarenanyuki. Sio umlete hapo Tabata mlipopanga. Hapo sio kwenu! Andaa nauli yako na atakaekusindikiza, nauli ya binti na mwenzie, na gharama za vinywaji na chakula siku hiyo. Utahitaji kama 700,000
3. Kifuatacho ITV ni kuwaalika wakwe zako nyumbani. Uwatoe watu kama nane Mwanza, uwalete Arusha. Wale, walale, wajisaidie, kwa gharama zako. We acha ubishi, tenga 800,000 tu.
4. Kwani we wazazi wako wanajua unakooa? Sasa je? Wasafirishe kwenda Mwanza! Watu watano. Utahitaji kuwa na 500,000. Beba pia ATM card yako, kuna imejensi.
5. MAHARI ndio topic inayofuata sasa. Ukiwa mjanja, unganishia kwenye hiyo safari hapo juu uue ndege wawili. Pamoja na hayo, itabidi ubebe 2,000,000.
6. Sasa kijana unaweza kumvisha mchumba wako pete. Nunua ya kawaida kabisa ya dhahabu. 350,000. Tukio lenyewe la kumvisha pete unaweza ita marafiki wawili watatu ukatumia 200,000. Au fanya sherehe kabisa. Mi simo
7. Oke, sasa unaweza kuitisha vikao vya harusi. Tengeneza kadi za mwaliko wa kamati kwa 200,000, kikao cha kwanza gharama zote ni juu yako. Andaa 500,000. Swali la kwanza kwenye kikao: "We una shing ngapi?" Sema 2,500,000.
8. Utahitaji 100,000 ya sms na simu kukumbushia michango. (Shukuru Mungu kuna cheka time)
9. Wakati vikao vinaendelea, utatuma 200,000 kwa m-pesa ili mambo ya kimila yaendelee kule nyumbani. We unaelewa
10. "Darling, sasa mi kwenye kitchen party ntavaa nini?" 300,000!
11. "Darling, kuna mahali nimeona gauni zuri la send." 400,000!
12. "Baby, rafiki yangu alinunua gauni la harusi China yani lilimpende..." 700,000!
13. Wakati huo wewe mwenyewe hujajua utavaa nini, hujanunua pete za harusi, hujamvalisha best man na mkewe. Tuseme unahitaji kama 1,500,000 maana utalia lia sana. Kumbuka, gharama hizi huchangiwi na kamati. Wala hutarudishiwa.
14. Siku ya send off lazma uende Mwanza. Utaenda mwenyewe? Ndugu wawili watatu na mshenga 600,000. Kwenye send off utatakiwa kutoa sijui blanketi la bibi, vitenge vya mashangazi, na vikorokoro kibao. Nunua hivyo vitu 300,000 uende navyo ili kupunguza gharama. Beba 200,000 za wale mashangazi watakaoibuka ghafla!
15. Mshonee baba mkwe suti 100,000 mama mkwe yeye atavaa gauni la 50,000.
16. Fotokopi hiyo hapo juu (namba 15) kwa wazazi wako. 150,000
17. Watu watakaopenda kuvaa sare wajitegemee! Mimi sina hela! Ila utavishonea nguo vile vitoto kwa 80,000.
18. Siku mbili kabla ya harusi, utaanza kupokea wageni. Unatakiwa uwatafutie malazi na chakula. Kwa ujumla utahitaji kama 500,000
19. Jioni watoe auti mashemeji zako ambao hawajawahi kufika Dar ukawanunulie bia ili wakuone wa maana. 200,000
20. Siku ya harusi bibi harusi na mwenzie na watoto na ma maids watatakiwa wakapambwe saluni. 200,000
21. We na mwenzio mtaenda kunyoa hapo kwa nanii. Ndevu na nywele na black kibishi 40,000
22. Siku ya harusi beba sadaka 10,000. Wakati huo umeshamtuma kijana akakulipie hoteli mtakayofikia baada ya harusi. Kamati haitoi hela hiyo, so utalipa malazi ya siku mbili 200,000
23. Kama mtaenda honeymoon sehemu yoyote nzuri nzuri nje ya mji, si chini ya 800,000 kwa angalau siku 5.
24. Wakati uko huko honeymoon, huna hata kumi, mwanakamati mmoja ambae hakuchanga anakupigia simu " Sasa tunavunja lini kamati?" Pesa yote iliyochangwa ilitumika kwenye harusi, sasa gharama za kuvunja kamati ni za nani?? 500,000! 25. SASA MNAANZA MAISHA YA UNYUMBA. 14,180,000 poorer. KAZI KWENU MSIOOA/MTAKAOOA TENA.KAM VIPI JIWEKE MAPEMA HAAA HAAAAAA HAAAAAA. FUATANA NAMI KATIKA
www.kingotanzania.blogspot.com

KINGO
0752-881456
KALI YA MWAKA 2012 HII HAPA
BABA ANAETUHUMIWA KUZINI NA KUZAA NA MWANAE WA KUMZAA ATINGA MAHAKAMANI BAADA YA KESI KUAIRISHWA AZOMEWA NA KINA MAMA NA KUKIMBIA KAMERA ZA WANDISHI WA HABARI
Bwana Yussuf Hamad anaetuhumiwa kuzaa na bintie akitaka kumpokonya kamera mwandishi wa gazeti la majira Rashid Mkwinda ili asimpige picha |
Jamaa kuona amezidiwa akaamua kujifunika na shati lake huku akitoa maneno makali kuwa nyie waandishi mmekosa cha kuandika mmeona hii ndiyo habari hakuna habari nyingine? alihoji mtuhumiwa huyo |
Huyoooo anatoka nje ya mahakama |
Sasa anavaa kofia yake ili watu wasimtambue huku akisema nifuateni niwaonyeshe kazi |
Njooni sasa huku kashika jiwe |
Kuona anazidi kufuatwa akaamua kuondoka mahali hapo huku akiwa na jiwe lake mkononi |
PICHA KWA HISANI YA JEM
No comments:
Post a Comment