 |
BAADHI YA VIJANA WA MCHUNGAJI MWALWEGA |
 |
MAREHEM PAUL LUKONGO KULIA SIKU ALIPOSIMAMIA HARUSI YA MDOGO WANGU BARAKA MWALWEGA |
 |
MAREHEM PAUL LUKONGO AKIWA NA BARAKA SIKU YA HARUSI KABLA YA KUELEKEA KANISANI NA ANAYEONEKANA KICHWA KWA CHINI NI CAROLINE KINGO |
 |
MAREHEMU PAUL LUKONGO NA MKEWE KATIKATI WAKIWA KATIKA PICHA NA BAADHI YA FAMILIA YA MWALWEGA SIKU YA HARUSI YA BARAKA HAWA NDUGU ZETU WALISIMAMIA HARUSI |
 |
MAREHEM PAUL LUKONGO NA MKEWE KULIA NA BARAKA NA MKEWE KUSHOTO SIKU BARAKA ALIPOKUWA ANABATIZA MTOTO WA KWANZA, HAPA WANAFURAHIA MATUNDA YA NDOA. MAREHEM |
Marehem Paul Lukongo amefariki saa 6 usiku wa kuamkia jumamosi tarehe 08.12.2012 baada ya kulalamika kichwa kuwa kinamuuma sana ndipo alipo kimbizwa hospitali ya Amana jijin Dsm na ndipo mauti ikamkuta baada ya masaa 4 kufikishwa Hospitalin hapo.
Leo usiku mkewe na marehem Paul anawasiri akitokea safari yake ya kikazi USA, ibada ya kumuaga marehem itafanyika Kanisa la KKT la Ubungo siku ya kesho asubuhi tarehe 11.12.2012 na baada ya kuaga mwili wa marehem safari ya kuelekea kijijini Ulyangulu wilaya ya Ulambo mkoa wa Tabora katika familia ya mzee Lukongo ndipo maziko yatafanyika.
Familia ya Mchungaji Mwalwega na wote tunaungana kuwapa pole mke wa marehem Tumpe na watoto wake Abigaili na Yvonne, wazazi wake na ndugu na jamaa kwa msiba mzito ulio tokea ghafra nasi katika mazishi hayo tutawakilishwa na Baraka pamoja na mkewe . Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina la Bwana na lihimidiwe. Ayubu.1:21C.
na
 |
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA DIWANI |
 |
MAREHEMU JOSEPH MWASOKWA
MNAMO TAREHE 09/12/2012 MAJIRA YA SAA
06:30HRS HUKO MAENEO YA BLOCK - T JIJI NA MKOA WA MBEYA. JOSEPH S/O NELSON
MWASOKWA, MIAKA 78,KYUSA, AFISA USALAMA WA TAIFA MKOA WA MBEYA [MSTAAFU] NA
MKAZI WA BLOCK T . ALIGUNDULIWA KUUAWA NYUMBANI KWAKE KWA KUKATWA NA KITU
CHENYE MAKALI KINACHODHANIWA KUWA NI PANGA NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA.
MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA NA MAJERAHA MAKUBWA SEHEMU ZA SHINGONI,
KICHWANI MABEGANI NA MKONO WA KUSHOTO. KATIKA TUKIO HILO HAKUNA
KITU CHOCHOTE CHA MAREHEMU KILICHOCHUKULIWA KWANI MAREHEMU ALIKUTWA NA PESA
TASLIMU TSHS 107,000/= DOLA 200 ZA KIMAREKANI NA SIMU MOJA YA MKONONI. MBINU
ILIYOTUMIKA NI KUMVIZIA WAKATI AKIINGIA KWENYE GETI LA NYUMBA YAKE. KWA MARA YA
MWISHO MAREHEMU ALIRUDI NYUMBANI NA JIRANI YAKE MAJIRA YA SAA 20:00HRS TOKA
SOWETO KUTAZAMA FAINALI YA MPIRA WA MIGUU KOMBE LA CHALLENGE KATI YA UGANDA NA
KENYA. CHANZO CHA MAUAJI HAYO BADO KINACHUNGUZWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MTU/WATU
WENYE TAARIFA JUU YA WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI WAZITOE KATIKA MAMLAKA
ZINAZOHUSIKA ILI HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE.
Signed By,
[DIWANI ATHUMANI – ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
pia
|
No comments:
Post a Comment