Bi. Kidude akiveshwa nishani na Rais Jakaya Kikwete Ikulu jana
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo mchana ametunuku nishani
kwa watu kutoka makundi mbalimbali yajamii waliotumikia taifa kwa
uadilifu na kutoa mchango wa pekee.Miongoni wa waliotunukiwa nishani jana
ni pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Jaji Mstaafu wa
Mahakama ya Rufaa Eusebia Munuo pamoja na Msanii Mkongwe Bi.Fatma Baraka
Khamis(Bi.Kidude).Wengine waliotunikiwa nishani ni pamoja na Watumishi
wa umma na askari Jeshi na Polisi.
Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, Eusebia Munuo akivishwa nishani
Rais jakaya Kikwete akimvisha nishani Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue ikulu Jijini Dar es Salaam.
Picha na IKULU
Majambazi Waipora hadi Maiti
Mhudumu wa chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya Mkoa Singida,
akirekebisha mapambo ya jeneza lililokiwa na mwili wa marehemu Munchari
Lyoba, mwanafunzi wa SUA , jeneza lililovunjwa na majambazi na maiti
kupekuliwa yakitafuta fedha zaidi baada ya kupora wasindikizaji. (Picha
na Gasper Andrew)
WATU wanaodhaniwa kuwa ni majambazi, wamevamia gari lililokuwa linasafirisha maiti kutoka mjini Morogoro kwenda mkoani Mara kisha kupora takriban Sh19.8 milioni walizokuwa nazo waombolezaji.
WATU wanaodhaniwa kuwa ni majambazi, wamevamia gari lililokuwa linasafirisha maiti kutoka mjini Morogoro kwenda mkoani Mara kisha kupora takriban Sh19.8 milioni walizokuwa nazo waombolezaji.
Katika tukio hilo la kusikitisha lililotokea juzi
mkoani Singida, majambazi hao walivunja vioo vyote vya gari pamoja na
jeneza lililokuwa na mwili wa Munchari Lyoba aliyekuwa mwanafunzi wa
mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) cha Morogoro na
kumpekua marehemu.
Akizungumza na waandishi wa habari jana nje ya
chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Mkoa wa Singida, mkuu wa
msafara uliokuwa ukisafirisha maiti, Makaranga alisema kuwa tukio hilo
lilitokea juzi saa 7:30 usiku katika gari aina ya Land Cruiser mali ya
SUA.
Akisimulia tukio hilo, Makaranga alisema kuwa
lilitokea katika Barabara Kuu ya Dodoma – Mwanza nje kidogo ya Mji wa
Singida kwenye kona maarufu kwa jina la Mohammed Trans kuelekea mkoani
Mara.
Alisema kuwa gari hilo pamoja na jeneza,
lililobeba viongozi wa wanafunzi sita na viongozi wengine wanne
lilipofika eneo la tukio, walikuta mawe makubwa yamepangwa barabarani na
kuwalazimisha kusimama ndipo wakavamiwa na kundi kubwa la vijana, ambao
walibeba bunduki mbili aina ya gobore, marungu, mashoka na mawe.
“Walipofika walipiga kioo cha gari letu kwa mbele
na kumparaza kwa panga usoni dereva wetu. Baada ya hapo walivunja vioo
vyote na kutuamuru kutoa kila kitu tulichokuwa nacho,” alisema
Makaranga.
Makaranga alisema kuwa katika tukio hilo, aliporwa
Sh2 milioni alizokabidhiwa azihifadhi kwa ajili ya kugharimia msafara
huo, Sh8.8 milioni zilizochangwa na wanafunzi kama rambirambi kwa
mwenzao na jumla ya Sh9 milioni ambazo wasindikizaji walikuwa nazo
mifukoni mwao.
“Pia tuliporwa simu zetu zote za mikononi, viatu, laptop na mabegi yote ya nguo zetu,” alisema.
Makaranga aliyeeleza kuwa anafanya kazi za
kiutawala SUA, aliwataja walioumizwa na majambazi hao kuwa ni pamoja na
yeye, dereva wao na kiongozi wa wanafunzi, Idd Idd ambao walitibiwa
katika Hospitali ya Mkoa wa Singida na kuruhusiwa.
Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mwalimu Queen Mlozi,
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa amewasiliana na
uongozi wa SUA ili watume gari lingine na kukarabati jeneza
lililoharibiwa na majambazi hao.
Mlozi aliongeza kuwa kwa ushirikiano wa Jeshi la
Polisi na Kamati ya Ulinzi na Usalama, watahakikisha watu waliofanya
unyama huo, wanakamatwa haraka iwezekanavyo ili waweze kufikishwa mbele
ya vyombo vya sheria.
MICHEZO
TIMU YA BUNGE SPORTS CLUB YA TANZANIA YAIKANDAMIZA BUNGE YA KENYA MAGOLI 5-0
Katika
mashindano haya ambayo hufanyika kila mwaka huyakutanisha mabunge ya
nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda. Waratibu wa michezo
hii ni Jumuiya pamoja na Bunge la Afrika Mashariki. Kwa mwaka huu
Burundi haikushiriki.
Chini
ya ukufunzi wa Naibu Waziri (TAMISEMI) Mhe. Kasim Majaliwa (Mb) .na
uongozi wa Mhe. Idd Azzan (Mb) mabao hayo yalifungwa na Mhe Amos Makala
(Mb), Yusuf Soka (2), Mark Tanda na Mhe. Joshua Nassari. (Na Prosper
Minja)
Tanzania
yaendeleza ubabe wa kwa timu za mabunge ya nchi za Jumuiya ya Afrika
Mashariki baada ya timu ya mpira wa kikapu wananwake kuinyanyasa Kenya
Bunge Sports Club kwa mabao 51-25. Wakati huohuo, timu ya wanaume
imeedelea kutoa adhabu kali leo ikiwa ni zamu ya Rwanda ambapo hadi
kipenga cha mwisho Tanzania 6 Rwanda 0. Jana Kenya ilibamizwa bao 5-0
No comments:
Post a Comment