Dk. Mwakyembe Nimeona Kazi Yako Leo Jijini Mwanza
![]() |
Jengo la Shirika la Reli Mwanza |
![]() |
Tangazo likionyesha kuanza kwa safari za gari moshi |
![]() |
Abiria wakishuka baada ya gari moshi kufika steshen ya mwanza |
![]() |
Raia wa kigeni nao walikuwa miongoni mwa abiria waliowasili na gari moshi |
![]() |
Waandishi wa habari wakizungumza na naibu waziri wa uchukuzi Dk. Charles Tizeba |
![]() |
Moja ya mabehewa ya Gari Moshi |
![]() |
Wananchi waliofika kushuhudia kufika kwa gari moshi kwenya stesheni ya mwanza |
![]() |
Moja ya behewa la gari moshi likiwa katika hali mbaya |
![]() |
Naibu waziri wa uchukuzi Dk. Charles Tizebaakitoka kuzindua safari za gari moshi |
![]() |
Salamu kwa Dk Mwakyembe |
Shikamoo
Dk Mwakyembe, habari ya Jumapili najua utakuwa umepumzika leo jumapili
baada ya majukumu ya wiki iliyopita , mimi rafiki yako Mkami Jr baada
ya kutoka kukusaidia kazi ya kukagua Reli ya Moshi, Nimeamua nisafiri
mpaka kanda ya ziwa nikusaidie tena kazi ya kukagua.
Dk
Mwakyembe najua utashangaa kwanini nimejipa kazi hii bila kupewa kibali
cha ofisi yako (Wizara ya uchukuzi), binafsi mimi nimejiajiri kufanya
kazi zote za umma hivyo nadhani hata kazi hii ya kuja mwanza kukagua
reli ni moja ya majukumu yangu kama mfanyakazi wa umma nisiye na ofisi
wala mshahara au posho ya safari Dk mwakyembe usije shangaa siku
nyingine nikafika hadi bandarini nikusaidie kupunguza msongamano wa
makontena kwa kazi hizi nazofanya sihitaji kusifiwa, sihitaji posho ila
nimeipenda tu kazi hii.
Dk
Mwakyembe kama ambavyo niliyoona hali ya reli kule Moshi ambapo
nilikuta Reli na majengo mabovu na behewa moja tu na sikuona dalili
zozote za reli ile kufanya kazi na wala sikuona matumaini kama kuna siku itafanya kazi.
Leo
hii Dk Mwakyembe umeniwahi huku Mwanza sina budi kukupongeza wewe na
timu yako kwa kazi nzuri kazi nzuri mnayofanya, leo nimeona Gari moshi
likifika stesheni ya Mwanza na nimeomuona Naibu Waziri wako Dk Dk.
Charles Tizeba akizungumzia ujio wa safari za Gari moshi huku akisema
maneno yenye kutia matumaini ikiwemo kuboresha usafiri huo kadri uwezo
unapopatikana ni maneno ya faraja naamini amezungumza kwa niaba ya ofisi
yako hivyo nawe unahusika kutekeleza aliyoyasema msaidizi wako,
Pamoja
na sifa ambazo wananchi wanakumwagia ila Rafiki yangu Dk Mwakyembe kazi
ngumu ipo mbele yako ndio maana nikaona nikusaidie baadhi ya mambo ,
Jambo kubwa ambalo wananchi wamekuwa wakizungumzia usafiri huu ambao
kwao ni ukombozi ni jambo la kuhujumiwa , mfano leo nimesikia kuwa wenye
mabasi hutumika kuhujumu miundombinu ya reli na kufanya gari moshi
kusimama kufanya kazi mara kwa mara, Sina ushahidi kuhusiana na jambo
hili ila waswahili walisema lisemwalo lipo kama halipo laja..
Nikutakie
kazi njema Dk harrison Mwakyembe na msaidizi wako Dk. Charles Tizeba
na timu yako ya wizara ya uchukuzi na timu nzima ya Shirika la reli kwa
kazi nzuri mnayoifanya ila inabidi mjipange kukabiliana na changamoto
ikiwamo hujuma katika miundombinu na kuboresha magari moshi hapa nikiwa
na maana kukarabati injini za gari moshi na kukarabati mabehewa yawe ya
kisasa zaidi.
Asante
sana Dk Mwakyembe nikutakie mapumziko mema ya weekend na fikisha
salamu zangu kwa familia yako bila kumsahau dereva wako na kesho ukiwa
ofisini fikisha salamu zangu kwa Katibu Muhtasi wako hawa ni watu muhimu
pia kwenye kazi yako.
PICHA KWA HISANI YA Mkami Jr- (Mjengwa Blog-Mwanza)
LEO SIKU YA UHURU WA TANGANYIKA MIAKA 51
Rais
wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dk.Jakaya
Kikwete akiwasili katika gari maalum la Kijeshi na Mkuu wa majeshi
Jenerali Davis Mwamunyange kwenye uwanja wa uhuru kwa ajili ya
maadhimisho ya miaka 51 Uhuru wa Tanzania Bara 2012 yanayofanyika kila
mwaka Desemba 9, Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Mwaka huu ni “Uwajibikaji,
Uadilifu na Uzalendo ni nguzo ya Maendeleo ya Taifa letu”
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania Dk. Jakaya
Kikwete akikagua gwaride la vikosi vya Ulinzi na usalaama katika
maadhimisho hayo.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania Dk. Jakaya
Kikwete akikagua gwaride la vikosi vya Ulinzi na usalaama katika
maadhimisho hayo

Rais
wa Msumbiji Mh. Armando Guebuza akipokewa na Mkuu wa mkoa wa Dar es
salaam Mh Said Meck Sadik mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Taifa.
Rais
wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mh. Joseph Kabila akipokewa na
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Said Meck Sadik mara baada ya kuwasili
kwenye uwanja wa Uhuru asubuhi hii.
Mama Maria Nyerere akiwasili kwenye uwanja wa Uhuru kwa ajili ya kuhudhuria maadhimisho ya miaka 51 ya uhuru wa Tanzania.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Mizengo Pinda akiwasili
kwenye uwanja wa Uhuru kuhudhuria maadhimisho hayo huku akisindikizwa na
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Said Meck Sadik.
Vikosi
vya Ulinzi na Usalama vikiwa vimejipanga tayari kwa gwaride la utii na
heshima mbele ya Amiri jeshi Mkuu na Rais Jamhuri ya muungano ya
Tanzania Dk. Jakaya Kikwete.
Makamu
wa Rais Dk. Gharib Bilal akisalimiana na Mama Fatma Karume mara baada
ya kuwasili uwanjani hapo, katikati ni Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda.
Rais
Jakaya Kikwete akipokea gwaride la heshima wakati wa maadhimisho ya
miaka 51 ya uhuru wa Tanzania Bara yanayofanyika kwenye uwanja wa Uhuru
jijini Dar es salaam akiwa pamoja na viongozi mbalimbali kutoka nje na
ndani ya nchi
Rais
Dk. Jakaya Kikwete kulia akipokea Gwaride la Heshima lililpokuwa
likipita mbele yake wanaofuatia katika picha ni Rais wa Zanzibar Dk.
Mohamed Shein, Rais wa Namibia Mh. Ifikepunye Pohamba na Mke wa Rais
Mama Salma Kikwete wakiwa katika maadhimisho hayo
RAIS DK. JAKAYA MRISHO KIKWETE AONGOZA WATANZANIA KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 51 YA UHURU WA TANZANIA UWANJA WA UHURU
(PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWEBLOG.COM)
Viongozi mbalimbali wakiwa katika
maadhimisha hayo kutoka kulia ni Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo, Mama Maria Nyerere, Rais wa Msumbiji Mh. Armando
Guebuza,Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Gharib
Bilal na Mzee Ali Hassan Mwinyi rais Mstaafu wa awamu ya pili
Mkutano Wa SADC Wamalizika Na Maazimio Yatolewa Katika Mkutano Wa Wanahabari
Baadhi ya wapiga picha za televisheni mbalimbali kutoka nchi wanachama wa SADC wakichukua matukio |
Rais Kikwete (kushoto) akiagana na Katibu wa SADC Tomaz Salomao baada ya
kumalizika mkutano wa dharura wa SADC
Rais kikwete (kushoto) akijibu masuali ya waandishi wa habari, (kati) Mk wa SADC
Armando Guebuza (kulia)katibu wa SADC
katibu wa SADC Tomaz Salomao (kulia) akisoma maazimio ya kikao, (shoto ) Mk wa
SADC Rais Armando Guabuza wa Mozambique
Rais Jakaya Kikwete ( kushoto) akijibu masuali ya waandishi wa habari pichani
hawapo
na
MTOTO WA MIAKA SABA AACHIWA MTOTO MCHANGA NA MWANAMKE ASIYEJULIKANA MBEYA
Kazi kweli kweli watoto wakimwimbia wimbo wa kumtania sharifu kuwa kapakaziwa mtoto |
Kwakweli tulikuta watoto wa shule ya msingi Mbata wamechangamka sana na kutupokea vizuri |
Sharifu huyo katikati jamani sasa mwachieni tunashukuru kwa kutuletea tuongee nae |
Rafiki yetu sharifu tayari wenzake wamemwachia na anaanza kutupa kisa cha kuachiwa mtoto mchanga |
Upendo Mwakipunda mwalimu wa shule ya msingi mbata amekiri kutokea kwa tukio hilo kweli walimpokea mtoto huyo na kumpeleka kituo cha polisi |
Mwaisango mpiga picha wa tulio hili na mtoto sharifu baada ya kuongeanae habari wakiwa katika pozi la picha |
![]() |
Kwa ujumla baada ya kumaliza maongezi tulianza kuona jinsi watoto wakiwa katika michezo mbalimbali shuleni hapo dogo katulia dirishani mwa darasa lake huku akipata embe kwa raha zake |
![]() |
Wengine madirishani wengine wanachora ukuta ni furaha tu shuleni hapo |
![]() |
Wa kuruka kamba haya wa kucheza mpira sawa |
Wanafunzi wakifurahia chandarua walichobuni shuleni hapo |
Wakifurahia kutembelewa shuleni kwao (picha kwa hisani ya jem mwaisango) |
KAMPENI YA VITA DHIDI YA UKIMWI,
Afisa
Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu akitoa muhtsari kwa
waandishi wa habari juu ya Taarifa kuhusu Mpango wa Umoja wa Mataifa
wa Msaada wa Maendeleo UNDAP 2011-2015 ambao unaelezea ushiriki wa Umoja
wa Mataifa katika kuendeleza nyanja mbalimbali ikiwemo kupunguza
umaskini wakati wa Semina ya kuwapa uelewa waandishi wa habari juu ya
Haki za Binadamu tukielekea kwenye maadhimisho ya Siku ya Haki za
Binadamu Duniani itakayoadhimishwa tarehe 10 Disemba mwaka huu.
Mwezeshaji
wa Semina hiyo Katibu wa Jukwaa la Wahariri nchini Neville Meena akitoa
changamoto kwa wanahabari kutumia fursa mafunzo hayo katika kuhabarisha
jamii kuhusu kazi zinazofanywa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa
nchini.
Mwakilishi Msaidizi wa UNICEF Bw. Paul Edwards akielezea nia ya Umoja
wa Mataifa kuwakutanisha waandishi wa habari kila mwaka katika semina za
mafunzo ambapo amesema jitihada za Umoja huo kutoa mchango katika
juhudi endelevu za kupunguza umaskini na kupatikana kwa haki za Binadamu
kulingana na visheni ya Maendeleo ya Taifa la Tanzania.
Mtalaam wa Program wa UNDP Bw. Amon Manyama akiwasilisha kwa wanahabari
mpango kazi maalum wa miaka minne unaojulikana kama United Nations
Development Assistance Plan 2011-2015 (UNDAP) uliotenga dola za
Kimarekani Milioni 777 kwa Serikali ya Tanzania mpaka kukamilika ifikapo
2015.
Mratibu
wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa yasiyo na ukazi hapa nchini Bi. Aine
Mushi akizungumzia jinsi mashirika hayo yanvyoweza kufanya kazi kwa
pamoja 'Delivering As One' na Mashirika ya Umoja wa mataifa yenye ukazi
hapa nchini.
Pichani Juu na Chini ni Washiriki wa Semina ya siku moja kutoka vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini.
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mh.
Mahfoudha Alley Hamid akizungumzia haki za msingi za Binadamu na wajibu
wa vyombo vya habari katika kutetea haki hizo na kufichua pale
zinapokiukwa ikiwemo kufuata maadili.
Afisa Mipango Mwandamizi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) Bw. Anthony
Rutabanzibwa akitoa somo jinsi waandishi wa habari wanavyotakiwa
kuripoti masuala yanayohusu hakiza Binadamu bila kutoka nje maadili ya
kazi zao.
Pichani Juu na Chini ni baadhi ya washiriki wakichangia mada na kutoa maoni wakati wa semina hiyo.
Mwenyekiti
wa timu ya Mawasiliano ya Umoja Mataifa Bw. Yusuph Al Amin wakati wa
semina hiyo akifafanua jinsi sekta ya mawasiliano vikiwemo vyombo vya
habari inavyoweza kuchangia maendeleo na kufanikisha kufuatwa kwa haki
za binadamu.
Afisa
habari wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi.Usia Ledama
akitoa changamoto kwa wanahabari kusoma makabrasha yanayotolewa na
mashirika mbalimbali ya umoja wa mataifa wakati wa mikutano na semina za
kuelimishana kuhusiana na masuala mbalimbali yanayohusu jamii kwani kwa
kufanya hivyo ndivyo watakavyoeweza kuelewa ushiriki wa Umoja wa
Mataifa katika kupunguza umaskini na kutetea haki za binadamu.
Baadhi ya Maofisa wa Umoja wa Mataifa na Wanahabari wakati wa Semina hiyo.
|
No comments:
Post a Comment