KUPITIA UKURASA WA FACEBOOK WA MH.SUGU
NATANGAZA VITA NA MADAKTARI: MARA ZOTE NIMEKUWA MSTARI WA MBELE KWA KUTETEA HAKI NA MASLAHI YA MADAKTARI WETU BUNGENI,LAKINI KWA NIABA YA WANANCHI WA MBEYA LEO NATANGAZA VITA NA MADAKTARI WA HOSPITALI YA RUFAA-MBEYA KITENGO CHA MIFUPA,WAMENICHOSHA KWA RUSHWA AMBAYO IMEKITHIRI KAMA AMBAVYO SIJAWAHI KUONA MAHALI POPOTE.WANANCHI MASKINI WANALAZIMISHWA KULIPA TSHS 300,000/= MPAKA TSHS 500,000/= KWA AJILI YA KUWEKEWA JUST A ‘P.O.P’, AU VINGINEVYO MGONJWA ANAAMBIWA ANA TATIZO KUBWA LINALOHITAJI OPERESHENI NA KWAMBA AENDE PERAMIHO AU MUHIMBILI-DAR…KUNA TAARIFA KUWA KUNA WANANCHI WENGI WAMEKUFA NA WENGINE KUKATWA MIKONO NA MIGUUU KWA KUWA TU HAWAKUWA NA FEDHA ZA KUWAPA MADAKTARI HAO WA RUFAA-MBEYA…SASA KWA KUWA NIMEJARIBU SANA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI AKIWEMO RC MH. KANDORO BILA MAFANIKIO KWA MADAI KUWA HAKUNA USHAHIDI,SASA WAKIENDELEA KUKAA KIMYA NA WATU WETU WANAENDELEA KUTESEKA NA KUFA BASI TUTALAZIMIKA KUTUMIA NGUVU YA UMMA KUJITETEA KAMA KAWAIDA YETU….
Msanii Sajuki Aanguka Jukwaani- Arusha
Msanii
wa filamu nchini,Juma Kilowoko akiwa ameshikwa na wasanii wenzake mara
baada ya kuanguka jukwaani juzi ndani ya uwanja wa Sheikh Amri katika
tamasha la wasanii wa muziki wa kizazi kipya na wale wa filamu.
Msanii huyo akitafakari kwa kina mara baada ya kuanguka chini ya jukwaa huku wenzake wakimpa pole.
Msanii
wa filamu nchini,Juma Kilowoko akiwa ameshikiliwa na wenzake
wakimshusha chini ya jukwaa mara baada ya kuanguka alipopewa nafai ya
kuwasalimia mashabiki wake
Na: Mahmoud Ahmad,Arusha
HALI ya msanii wa filamu
nchini,Juma Said Kilowoko maarufu kama Sajuki imeelezwa si ya kuridhisha
mara baada ya msanii huyo juzi kuanguka jukwaani mara baada ya
kuishiwa na nguvu wakati alipopewa kipaza sauti kuwasalimia mashabiki
waliofurika kumtizama.
Tukio hilo lilitokea juzi
jumapili katika tamasha la wasanii wa filamu na wale wa muziki wa kizazi
kipya lililofanyika ndani ya uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid
wakati msanii huyo alipopandishwa jukwaani kuwasalimia mashabiki wake.
Mara baada ya msanii huyo
kupandishwa jukwaani alipewa kipaza sauti ili aweze kuwasalimia
mashabiki wake lakini katika hali ya kawaida alifanikiwa kutamka neno
moja tu”ahhh” na kisha kudondoka chini ya jukwaa lakini kabla ya kutua
chini alidakwa na wasanii waliokuwa pembeni yake.
Hatahivyo,wasanii hao
walimkalisha chini ya jukwaa hilo ili aweze kupumzika na kisha baada ya
muda mfupi walimshusha chini ya jukwaaa hilo ili aweze kupata muda wa
kupumzika zaidi.
Akihojiwa na gazeti hili muda
mfupi mara baada ya kushuka jukwaani Sajuki kwa sauti ya upole alisema
kwamba hali yake kiafya si nzuri kwa kuwa hana nguvu na anahitaji
matibabu zaidi.
”Kaka hali yangu si nzuri kabisa naumwa sana sijisikii vizuri”alisema Sajuki huku akionekana mnyonge zaidi
Hatahivyo,baadhi ya mashabiki
waliokuwa wamefurika uwanjani hapo walionyeshwa kustushwa na hali ya
msanii huyo huku wengine wakiwatupia lawama nzito baadhi ya wasanii wa
filamu nchini walioambatana na msanii huyo kwa madai kwamba wanamtumia
ili wapate pesa ilhali mwenzao ni mgonjwa.
Wakihojiwa kwa nyakati tofauti
mashabiki hao kwa jazba walisema kwamba msanii huyo alipaswa kupewa muda
mwingi wa kupumzika kuliko kuambatana na wenzake mikoani kwani hali
hiyo inamchosha zaidi.
“Hawa watu wa Bongo movie ni
watu wa ajabu sana huyu mtu anaumwa sana sisi tunashangaa wanaambatana
na mtu mgonjwa mikoani wampe muda apumzike na si kumtumia kwa kupata
pesa”alisikika shabiki mmoja akiongea kwa jazba
na
Mwanamke Dereva Wa Basi La Shabiby
na
Mwanamke Dereva Wa Basi La Shabiby
NUSRA
Maguluko (28) ni msichana jasiri na anayependa kujaribu na kupata
mafanikio ya majaribio yake bila woga wala kujali ni aina gani ya kazi
anayotakiwa kufanya yeye kama mwanamke na ipi asiyostahili kufanya yeye
kama mwanamke.
Ni
ujasiri wake hasa ndiyo ulimuwezesha kumfikisha hatua aliyonayo kwa
sasa, ambaye ni miongoni mwa wanawake wachache na hasa kwa Tanzania
waliopata kuifikia na kujiamini hadi kuwa na ujasiri wa kubeba roho za
watu zisizopungua 40 kila safari moja ya kwenda Dodoma ama kotoka Dodoma
kuja Dar.
Nusra
ni mzaliwa wa Mkoa wa Manyara katika wilaya ya Kiketo, na ni mtoto wa
nne kuzaliwa kati ya 12 wa familia ya baba yake mzazi mzee, Maguluko na
Elimu yake ni Kidato cha pili tu.
Alimaliza
elimu ya Msingi mwaka 1997, katika Shule ya Msingi Matui iliyoko
Wilayani Kiteto, baada ya kuhitimu elimu ya msingi alijiunga na elimu ya
Sekondari ambayo kwa bahati mbaya hakuweza kumaliza na kuishia Kidato
cha pili baada ya kusumbuliwa na maumivu ya kichwa mara kwa mara.
Nusra,
alishauriwa na madaktari kupumzika kwa muda wa miaka mitatu bila kusoma
ama kuwa akiangalia karatasi nyeupe mara kwa mara, jambo ambalo
lilimfanya kuamua kumsumbua Baba yake mkubwa, Hamis Mang'endi aliyekuwa
ni fundi wa magari ili amfundishe ufundi na udereva wa gari.
Baada
ya kumsumbua sana baba yake mkubwa, kwa kuwa akiripoti katika gereji
yake kila asubuhi na kushinda hapo huku akimfuatilia kila analofanya
katika magari, Mzee Hamis, baada ya kuona kuwa Nusra alikuwa na moyo wa
kweli wa kujifunza ufundi, aliamua kuanza kumfundisha ufundi hatua kwa
hatua.
Baada ya kumudu kidogo kishika Spana, Mzee Hamis, mwaka 1998, alianza
kumfundisha udereva, tena kwa kumfundishia katika gari aina ya Comb Volkswagen, ambapo baada ya miezi sita tu Nusra tayari alishamudu kuendesha gari na kutulia barabani.
Nusra
alipomudu kufanya vurugu za barabarani, alikabidhiwa na baba yake
mzazi, Canter ya Tani 3 na robo ili aweze kufanyia kazi ya kubebea
mizigo, huku akikodishwa ambapo alifanya kazi hiyo kwa muda wa miaka
miwili.
Hatimaye
mwaka 2001, Nusra, aliamua kuachana na kazi ya kuendesha Canter ya
kubeba mizigo na kuamua kuanza kazi ya kulima kwa Treka, ambapo alikuwa
akikodishwa na wakulima na alimudua kulima hadi Heka 10 kwa siku kwa
ujira wa Sh. 10, 000 kwa kila heka moja.
Mwaka
2003, Nusra alianza kuendesha Min Bus, huku akiwa na Leseni ya Clac C
baada ya wakati huo kudanganya umri ili aweze kupata uhalali ya kufanya
kazi anayoipenda ya udereva.
Alifanya
kazi hiyo ya kutoa huduma usafiri kwa abiria kutoka Wilaya ya Kiteto
kwenda Vijijini hadi mwaka 2006, alipokabidhiwa Basi aina ya Fuso lenye
uwezo wa kubeba abiria 40, nakutoa huduma hiyo ya usafirishaji wa abiria
kutoka Wilaya ya Kiteto hadi Dodoma, kazi aliyoifanya hadi mwaka 2011.
Baada
ya kuchoshwa na njia za Vijijini na kile alichodai kuaua kutafuta
maslahi zaidi, Nusra, aliamua kuvaa, Mbunge wa Gairo, he Shabiby, na
kumuomba kazi jambo ambalo lilimshangaza na kumuhoji kama anaweza kweli
kuendesha gari kubwa tena la abiria.
''Baada
ya kuniuliza swali hilo, mimi nilimjibu Mheshimiwa samahani wewe
nisaidie unipe kazi, halafu ndiyo utaniona nikiwa kazini kama naweza ama
siwezi, kwani najiamini na ndiyo maana nimekuja kwako''. alisimulia
Nusra
Baada
ya maongezi marefu ya maswali na majibu juu ya ujasiri wa Binti huyo,
aliyeonekana mdogo akiwa na maelezo ya mambo makubwa, Mhe. Shabiby,
aliamua kumwajiri, Nusra ambapo hadi sasa anapiga mzigo katika kampuni
hiyo ya Shabiby, akiburuza Basi linalofanya safari zake Dar-Dom.
Hivi
Sasa Binti huyo, anandoto za kufungua Chuo cha Mafunzo ya Udereva kwa
wanawake, akiwa na lengo la kuwafikisha mbali wanawake wenzake ili
waweze kuwa na ujasiri wa kuendesha magari makubwa na si gari ndogo
pekee.
Kwa
hatua hiyo sasa Nusra, ameanza kusaka wafadhili, ili aweze kutimiza
ndoto zake hizo, ambapo amewamba wadau mbalimbali pamoja na Serikali
kujitokeza kumsapoti, ili kufanikisha kufungua chuo hicho chenye lengo
la kuwainua Kinamama.
No comments:
Post a Comment