Lema arudi mjengoni, kwa habari zaidi endelea kusoma mjengwa blog baadae |
Daktari Wa Rufaa Mbeya Atiwa Mbaroni Kwa Madai Ya Kupokea Rushwa
DAKTARI wa kitengo cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa Mbeya,Paul Kisabi (32), anayetuhumiwa kwa kupokea rushwa ya sh 100,000 |
Hapa daktari huyo akiwa na maafisa wa takukuru wakiingia mahakamani |
Hapa Dr huyo akiongea na wakili wake |
DAKTARI
wa kitengo cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa Mbeya,Paul Kisabi (32),
amefikishwa katika Mahakama ya Mkoa wa Mbeya, akikabiliwa na mashitaka mawili
ya kushawishi na kupokea rushwa ya shilingi 100,000 kutoka kwa mgonjwa
aliyefikishwa Hospitalini hapo baada ya kupata ajali.
Hatua hiyo imekuja baada ya Taasisi ya kuzui na Kuipambana na rushwa nchini takukuru, kumtia mbaroni daktari huyo juzi kwa tuhuma za kupokea rushwa ya kiasi hicho cha fedha baada ya kumuwekea mtego. Daktari huyo Kisabi amepandishwa kizimbani majira ya saa 3:45 na kusomewa mashitaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Mbeya, Fransis Kishenyi, aliyepangiwa kusikiliza kesi hiyo ambayo imeibua hisia kali kwa wananchi.
Katika kesi hiyo namba 237 ya mwaka 2012, upande wa mashitaka
uliongozwa na waendesha mashita wawili wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na
rushwa nchini (TAKUKURU), Joseph Mulebya na Nimrod Mafwele.
Waendesha mashitaka
hao walidai kuwa Disemba 19 majira
ya asubuhi akiwa katika sehemu yake ya kazi katika kitengo cha upasuaji,
mshitakiwa alitenda kosa la kwanza la kushawishi rushwa ya shilingi 200,000
kutoka kwa mgonjwa Meshack Brown, aliyefika hapo kwa lengo la kupatiwa
matibabu.
Walisema katika
kosa la pili, siku hiyo majira ya saa nane mchana akiwa katika baa moja iliyojulikana kwa jina la
Victoria iliyopo Jijini hapa, mshitakiwa alitenda kosa lingine la kupokea hongo
ya shilingi 100,000, huku akijua kuwa vitendo vyote hivyo ni kinyume na sheria.
Walisema kuwa kwa
mujibu wa sheria za taasisi hiyo,
makosa yote yaliyotendwa na mshitakiwa yanaangukia kwenye kifungu cha 15 ibara
ya 1 (a) cha sheria ya kuzuia rushwa namba 11 ya mwaka 2007.
Kabla kupangwa tarehe ya kutajwa tena kesi hiyo,
Wakili wa mshtakiwa huyo,
Ladislaus Rwekaza,aliiomba mahakama impe dhamana mteja wake akidai kuwa makosa
yanayomkabili yanadhaminika.
Hakimu Kishenyi alikubaliana na maombi ya Wakili Rwekaza kuwa mashtaka yote
yanayomkabili mshtakiwa yanadhaminika na kusema dhamana yake iko wazi.
Alimtaka mshtakiwa
huyo kutimiza masharti ya kuwa na
mdhamini mmoja ambaye atasaini mali yenye thamani ya Sh,500,000, na kwamba awe
na utambulisho wa barua kutoka kwa kiongozi wa serikali ya mtaa .
Hata hivyo mahakama ililazimika kuahirishwa kwa
muda wa dakika 20 ili kutoa nafasi kwa
mdhamini wa mshitakiwa kuleta barua hiyo baada ya kudai kuwa alikuwa ameisahau
kwenye gari lililokuwa nje ya jingo la mahakama.
Baada ya kupokea
ombi hilo hakimu Kishenyi
aliwahoji waendesha mashitaka kama wameridhika na hoja, ambao kwa pamoja
walikubali kwa maelezo kuwa dhamana ni haki ya kisheria kwa mshitakiwa hivyo
hawakuwa na pingamizi.
Mshitakiwa aliweza kutimiza masharti ya dhamana hiyo na
hivyo kuachiwa huru hadi januari 7 mwaka 20013 ambapo kesi hiyo itaendelea
kusikilizwa katika mahakama hiyo.
Kwa mujibu
wa kumbukumbu za mahama hiyo, mshitakiwa huyo Daktari Kisabi ni mmoja wa
mashahidi wa kesi nyingine inayoendelea mahakamani hapo ya mtoto Anethi
anayedaiwa kuchomwa moto katika mkono wake, kufungiwa ndani na kulazimishwa
kula kinyesi chake na Shangaziyake
Habari na moses
picha Mbeya yetu
Jeshi La Polisi Latoa Siku Saba Kwa Baadhi Ya Askari Wanaodaiwa Kuiba Milioni 150 Zilizo Porwa
Akizungumza na waandishi wa
habari jijini, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum, Suleiman Kova, alisema
kutokana na tuhuma hizo jeshi hilo limeunda Jopo la wapelelezi ili
kujua ukweli wa madai hayo.
Alisema Jopo hilo litaundwa na
watu watano, likiongozwa na Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum, Ahmed
Msangi, atakayehakikisha kwamba muda mfupi inavyowezekana, ukweli
upatikane ili wananchi wajulishwe matokeo.
Kamanda Kova alisema jeshi hilo
lina mfumo wake wa kuchunguza askari wake inapotokea amejihusisha katika
matukio yanayokwenda kinyume na maadili ya kazi yake.
Alisema tukio hilo halikubaliki
hivyo kila aliyepewa jukumu la kulifuatilia ni lazima ahakikishe kuwa
anafanya kazi kwa ufasaha ili majibu yapatikane haraka kuondoa shaka
shaka kwa wanachi.
Kova alimtahadharisha Msangi
kuwa, endapo atashindwa kutoa majibu ya kuridhisha basi atambue hata
yeye itabidi awajibike ambapo alisema vitu kama hivi vikiachwa viendelee
vinaliletea jeshi hilo sifa mbaya na kupoteza imani kwa wananchi.
“Pamoja na kumkabidhi kazi hiyo
Msangi lakini hata mimi sitakaa kimya bali nitalifuatilia kwa karibu ili
mradi tuwapatie wananchi ukweli”alisema Kova.
Alibainisha kuwa hawezi kupinga
kama askari wanaweza kushiriki katika vitendo hivyo viovu bali suala
hilo bado linahitaji ushahidi zaidi hivyo, ni vema wananchi wenye
ushahidi wakatoa ushirikiano utakaosaidia kupatikana fedha hizo.
Aidha, Kova alilitaka jeshi la
polisi kufanya kazi zake kwa nidhamu, uaminifu na ueledi kwani endapo
ofisa au askari atakiuka maadili ya kazi yake, basi hatua madhubuti
zitachukuliwa dhidi yake bila kuchelewa.
Hata hivyo, katika hali ya
kushangaza jopo hilo linaundwa na polisi wenyewe bila kushirikisha wadau
wengine kwa madai kuwa, eti lifanya kazi kwa kutii sheria zote bila
kwenda kinyume.
SERIKALI YATANGAZA MATOKEO YA DARASA LA SABA
|
No comments:
Post a Comment