MUONEKANO WA MLIMA RUNGWE LEO |
MUONEKANO WA MLIMA KYEJO NA MAJENGO YANAYOONEKANA NI MAANDALIZI YA CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA TUMAINI KINACHOJENGWA NA KKKT DAYOSISI YA KONDE |
BAADHI YA MAJENGO YA MADARASA YANAYOENDELEA KUJENGWA YA CHUO KIKUU |
Gesi; Tunagombania bakuli za supu, ng’ombe hajachinjwa!
Ndugu zangu,
Kwenye
jamii yetu kuna mjadala wa gesi. Kila ninapoufuatilia mjadala huu
naiona hulka ya baadhi ya viongozi wetu inavyodhihiri; kuwa
wanachanganya siasa na gesi. Kuna hatari ninayoiona ya nchi kulipuka. Ni
wanasiasa walioelekeza mjadala wa gesi ubebe sura ya kimaeneo na
kikabila. Na nahofia si muda mrefu tusasikia dini nayo ikichanganywa na
gesi. Hapa kuna tatizo kubwa. Kinachokosekana ni ufahamu wa jambo zima
kuhusu rasilimali zetu za nchi na nani wa kumnufaisha.
pia
Aliyepiga picha na Lema jela miaka minne
Na: Daniel Mjema-Moshi
MTU
aliyepiga picha na Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema akiwa amevalia
sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), amehukumiwa kifungo cha
miaka minne jela. Abubakari Kikulu (29), alipiga picha na mbunge huyo
Desemba 23 mwaka jana, baada ya Lema kumaliza kuhutubia mkutano wa
hadhara eneo la Mererani, ikiwa ni sehemu ya mikutano aliyoifanya
kutokana na Mahakama ya Rufani Tanzania kumrejeshea ubunge wake.
Maelfu wafeli kidato cha pili
Waziri wa Elimu Phlip Mulugo
WIZARA
ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imetangaza matokeo ya Mtihani wa Kidato
cha Pili mwaka 2012, yanayoonyesha kuwa wanafunzi 136,923 kati ya
386,271 waliofanya mtihani huo wamefeli.Katika matokeo hayo shule kumi
zilizofanya vibaya zote ni za Serikali, zikitoka Mikoa ya Kusini.
Wanafunzi kumi bora wakitoka katika shule binafsi na taasisi za dini,
ambapo Mkoa wa Dar es Salaam ukiongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya
wanafunzi waliofeli. Akitangaza matokeo hayo jijini Dar es Salaam jana,
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philip Mulugo alisema idadi
ya waliofeli ni sawa na asilimia 35.5, wakiwamo wasichana 74,020 na
wavulana 62,903, kwamba waliofaulu ni wanafunzi 245.9,32
Hata hivyo, alisema kuwa wanafunzi waliofeli watarudia kidato cha
pili na watapewa fursa nyingine ya kurudia mtihani huo na iwapo watafeli
tena watarejeshwa nyumbani.
Kwa mujibu wa matokeo hayo, Shule za St Francis ya mkoani Mbeya na Kaizirege ya Bukoba, mkoani Kagera zimetoa wanafunzi kumi bora, kati ya hao mwanafunzi wa tatu na nne pekee wakitoka Sekondari ya Kaizirege na waliobaki ni St Francis.
“Wizara imeamua wanafunzi hawa warudie tena kidato cha pili na watajiunga na wenzao wanaoingia kidato cha pili mwaka huu kuendelea nao kidato cha tatu mwakani, hivyo basi nawaomba wazazi wawape ushirikiano wa kutosha ili wajisijione wapweke hatimaye wakakata tamaa ya kusoma,” alisema Mulugo.
Hata hivyo, alisema kuwa matokeo hayo yanaonyesha kuwa katika mwaka huu, kiwango cha ufaulu kimepanda kutoka asilimia 45.4 ya mwaka 2011 na kufikia asilimia 64.5 mwaka huu ambapo watahiniwa 249,325 wataendelea na masomo ya kidato cha tatu.
“Wanafunzi waliofaulu ni sawa na asilimia 64.55 ambapo kati yao wasichana ni 133,213 na wavulana ni 136,122,” alisema Mulugo na kuongeza:
“Waliopata alama A, B na C walikuwa 127,981 na waliopata kiwango cha chini ya hapo ni 121,344, alama ya juu ya ufaulu ni asilimia 92.”
Alisema wanafunzi wote waliofanya mtihani huo, wasichana ni 187,244 na wavulana ni 199,027.
Kusini hoi
Matokeo hayo yanaonyesha kuwa shule za Serikali zilizofanya vibaya na kushika nafasi 10 za mwisho zinatoka Kanda ya Kusini. Alizitaja shule hizo kuwa ni ya Mihambwe, Diduma, Kiromba, Marambo, Mbembaleo, Kinjumbi, Litupi, Luagala, Miguruwe na Napacho.
Matokeo hayo pia yanaonyesha kuwa shule zisizo za Serikali zilizofanya vibaya mbili zinatoka Kanda ya Kusini, tano kanda ya Mashariki na mbili Kanda ya Kati. Shule hizo ni Mfuru, Pwani, Doreta, Kigurunyembe, Ruruma, At-taaun, Jabal Hira Seminari, Mkono wa Mara, Kilepile na Kiuma. Alisema kutokana na shule nyingi za Kusini kufanya vibaya, Serikali inaangalia uwezekano wa kupeleka walimu zaidi.
Kwa mujibu wa Mulugo, Mkoa wa Dar es Salaam unaongoza kwa kuwa na wanafunzi wengi waliofeli mtihani huo, licha ya kuwa na walimu wa kutosha tofauti na mikoa ya Kusini.
No comments:
Post a Comment