Tuesday, February 5, 2013

LEO TUKUYU KUMEKUCHA VYEMA JAPO MAPEMA KULIKUWA NA MGOGORO WA USAFIRI WA SAFARI ZA KWENDA MBEYA TUKUYU MADELEVA WA MABASI WALIGOMA KULIPA USHURU ILI KUSHINIKIZA UONGOZI WA HALMASHAURI KUTATUA KELO ZILIZOPO STANDI KUU YA WILAYA IKIWEMO YA KUTOKUWEPO NA CHOO NA KUPELEKEA WATU KUJISAIDIA HOVYO KATIKA MAENEO HAYO LAKINI HADI SASA MGOGORO HUO UMEKWISHA NA SHUGHURI ZINAENDELEA VIZURI

LEO TUKUYU
MOJA YA STUDIO YA UTANGAZAJI

MR LEBI G. MWAKATOBE AMESEMA KUWA HATUA YA KUMALIZIA UFUNGAJI WA MTAMBO WA RADIO YA KISASA CHAI FM UKO HATUA YA MWISHO NA MAMBO YALIYOBAKI NI YA UTEKLEZAJI WA NDANI ILI KUFANIKISHA CHAI FM KUFANYA KAZI  HIVYO AMEWATAKA WANANCHI KUKAA MKAO WA KUPATA MATUKIO ,HABARI , MICHEZO NA BURUDANI KUTOKA CHAI FM

CHAI FM HAPA NDIPO MTAMBO NA STUDIO ZINAPOFUNGWA.                                                CHAI FM NI REDIO YA KWANZA KUANZISHWA KATIKA MJI WA TUKUYU WILAYANI RUNGWE WAKULIMA WADOGO WA CHAI KWA UMOJA WAO WA RSTGA WAMEONA NJIA KUU YA MAWASILIANO NI KUANZISHA REDIO ILI KUONGEZA CHACHU YA MAENDELEA VIJIJINI MAANA ITASAIDIA KUPATA HABARI KWA WAKATI ZINAZOWAHUSU. MAANA WILAYA YA RUNGWE NI MAARUFU KWA KILIMO CHA CHAI, NDIZI, MAPARACHICHI,COCOA, MPUNGA, NA MAZAO MENGI YA MBOGAMBOGA

BAJAJI F.C YAZINDULIWA MBEYA WAPEWA JEZI MIPIRA NA VIATU

Timu ya Umoja wa Vijana  waendesha Pikipiki za magurudumu matatu Mkoani Mbeya imezinduliwa hivi katibuni na kupewa msaada wa jezi viatu na mipira toka kwa mlezi wao Mwaka Mwakisu hapo mlezi huyo akimkabidhi jezi mwenyekiti wa bajaji mkoa wa mbeya Iddi Ramadani 
Mlezi Mwaka Mwakisu akimkabidhi mipira mwenye kiti wa bajaji mkoa wa mbeya
Hapa mgeni rasmi Mwaka Mwakisu akiangalia jina la timu ya waendesha bajaji mara tu baada ya kukabidhi vifaa hivyo vya michezo kwenye ofisi za waendesha bajaji isanga jijini mbeya
Mlezi wa waendesha bajaji mkoa wa Mbeya Mwaka Mwakisu amewataka wanaumoja huo wa bajaji kutumia vifaa hivyo vya michezo  kuleta mshikamano kwenye michezo na afya zao pia na kuacha kushabikia mambo ya kuleta vurugu na kuvunja amani ya mkoa wa mbeya na Tanzania kwa ujumla  
Mwenyekiti wa bajaji mkoa wa Mbeya akimshukuru mlezi wako wa kuwasaidia vifaa vya michezo na kuzindua timu yao ya waendesha bajaji mkoa wa Mbeya
Mgeni rasmi akipandisha bendera ya timu ya Bajaji FC kuashiria kuzinduliwa kwa timu hiyo
 

 

TAMKO LA WALIOKUWA VIONGOZI WA CHADEMA - MBEYA, KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA KUHUSU KUHAMIA NCCR-MAGEUZI TAREHE: 03/02/2013.

Moses Aliko Mwasubili (bulldozer)

Sarah A. Mwaseba


Ndugu wanahabari, salaam!
Ndugu wanahabari, Kwanza hatunabudi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa ulinzi anaotupatia na uwezo wa kutambua fikra zetu. Tunawashukuru viongozi wetu wa NCCR - Mageuzi kwa kututambua na kufika Mbeya ili kutupokea. 
Pia tunawashukuru waandishi wa habari wote kwa kazi nzito inayowafanya muwe maadui na marafiki katika utekelezaji wa majukumu yenu kwa Taifa letu. Mungu na awajalie ulinzi mkuu katika kutekeleza majukumu yenu.   
Ndugu Wanahabari,  
Sisi ni sehemu tu tunaohamia NCCR-Mageuzi kutoka CHADEMA na vyama vingine. Kimsingi tumetangulia na tumeamua kujitokeza mbele ya watanzani kupitia kwenu wanahabari ili kuwa mashuhuda wa kisiasa
Wapo wenzetu wanaohama kimya kimya kimwili na kifikra. Lakini wapo wengine tuliowaacha huko kwenye matawi yetu tunakwenda kuwapokea na kuanza nao kazi mpya katika Demokrasia ya kweli na mfumo bora wa kiutawala ndani ya NCCR Mageuzi.
Wapendwa wanahabari, harakati zetu zina historia tofauti katika siasa za nchi hii. Wapo ambao leo hii wanarudi NCCR baada ya kuhama miaka kadhaa iliyopita. 
Lakini wapo pia wanaotoka  CCM na CUF. Lengo letu ni kuitoa CCM madarakani na kujenga utawala wa sheria na Demokrasia ya kweli ndani ya vyama vyetu. 
Kwa furaha kubwa kabisa tunapenda kuchukua fursa hii kuwatangazia wana Mbeya na umma wa Watanzania kwa kuvunja ukimya na sasa  tunatangza rasmi kujiunga na Chama Cha NCCR- Mageuzi ( National Convention For Construction and Reform- Mageuzi) na tunasema tena kuwa, tumejiunga kwa hiari yetu kutokana na kuikimbia CHADEMA kwa mambo yake ambayo kwa uchache tunayaeleza kama ifuatavyo:
·         Uongozi wa kitaifa umefeli kujenga demokrasia ya kweli ndani ya chama kwa kukumbatia ufisadi wa kutumia vibaya ruzuku ya chama. 
Chadema mikoani imebaki ni kujichangisha fedha kwa kila tukio la ujenzi wa chama utadhani hakuna pesa za ruzuku na michango ya wafadhili.
·         Uongozi mbovu wa Mhe; Mbowe na dk. Slaa kwa kushindwa kusimamia katiba ya chama katika kutatua migogoro ya chama na kuishia kuwa na mbinu ya kufukuza wanachama wema kwa majungu wanayoyajenga wenyewe. 
·         A  tukisema ukweli wa ouvu wao jamii haiwezi kuamini. Wanajidanganya!!!!  Hii ni ishara ya kufinyanga katiba na kutoiheshimu dhana ya nguvu ya umma.
·         Chama kujaa utashi wa nguvu ya umma na kulazimisha maandamano, migomo kwa vitu visivyo na ulazima.
 Sisi hatuwezi kuamini pamoja na watu walio na malengo ya kuleta fujo kitaifa kwa kisingizio cha kutafuta ukombozi mpya wa taifa. 
·         Hatua ya kuwafukuza fukuza viongozi bila kuwasilikiliza hususani wa nyanda za juu kusini.
·         Dk. Slaa kulipwa mamilioni ya pesa kama mshahara wake na posho lukuki amejikusanyia na watu anaowataka Makao Mkuu. 
·         Akina mama Mbeya walihamasishwa kuwa tuwe tunampokea mchumba wa Katibu mkuu slaa kama mke wa raisi kumbe ni mwanachama wa kawaida anayetumia vibaya rasilimali za chama.
·         Uwezo mdogo wa kutekeleza ahadi alizoahidi mbunge wa mjini ‘joseph mbilinyi’ kwa wananchi wa mbeya. Ameacha kuufanya ubunge kuwa ni taasisi nyeti ya umma na ameamua kuutumia kama jukwaa la muziki na ameonesha Mbeya hatuna uwezo wa maendeleo ya pamoja.  
 Wakati wa kampeni aliahidi kujenga mabwawa ya samaki, bandari ya nchi kavu, vifaa vya hospitalini, benki ya wana Mbeya, umoja wa akina mama, vikundi vya ujasiliamali vya kijamii, kuinua wasanii wa mbeya, kulifanya jiji la mbeya liwe mfano wa kuigwa Tanzania. 
Pia aliahidi kutatua kero ya elimu (shule za kata), usafi wa jiji, mpango mzuri wa masoko ndani ya jiji. Lakini hadi leo hakuna anachofanya zaidi na hata bungeni na kupandikiza chuki za kukataa kupokea Raisi wa nchi anapokuwa na ziara mkoa wa mbeya. 
·         Mbunge ameendelea kuchochea wanachama asiowataka wafukuzwe nafasi za uongozi na anaowataka walindwe. 
Aliwahi mwambia DK, Slaa kuwa akimtoa mwenyekiti wa wilaya ya mbeya mjini basi, yeye anarudisha kadi; masikini bila kujua mzee wa watu dk. Slaa akamsikiliza na akageuka mbogo kwenye kikao cha ndani na kuamua kuwalinda waharifu wa siasa za Mbeya na kuwafukuza ambao ‘SUGU’ hawataki.  Dk. Slaa alionesha uwezo mdogo wa kudadavua mambo ya maneno ya majungu. 
Tumechukua uamuzi huu mzito wa kuhama chadema na kujiunga na NCCR-Mageuzi kwa kuwa NCCR kwa matendo kimeonekana kuwa chama cha UTU na chenye misingi bora ya usawa, uheshimu wa haki za wanachama na watanzania na chenye mshikamano wa kweli.
S/N
JINA MWANACHAMA
WADHIFA NDANI YA CDM
KATA/TAWI
1:
Moses Aliko Mwasubili (bulldozer)
Katibu mwenezi wa wilaya
Mbeya mjini
2:
Emmanuel Amani Mwangoka (Cash Money)
Mpambe wa mbunge/mwanachama
Mbeya mjini
3:
Magrethy John M ota
Mjumbe wa kamati tendaji
Kata ya Isyesye
4:
Hosea A. Mwangoje
Mjumbe kamati tendaji na MC Kampeni za mbunge – SUGU
Mbeya mjini
5:
Sarah A. Mwaseba
Mwenyekiti wa BAWACHA
Kata ya Isyesye
6:
Emmanuel Nehemiah Ngogo
Mwenyekiti
Tawi la Tawi
7:
William Swila
Katibu mstaafu wa Wazee
Mkoa wa mbeya
8:
Jonathani Mwakalinga
Katibu mwenezi  wa Kata
Kalobe
 Kimepitia migogoro mingi na ya kutisha lakini bado ni imara na hivyo ni vema watanzania wakajenga imani na chama Komavu kuliko CHADEMA ya watu wachache na iliyo furika majungu na ukabila pia haina ukomavu na uzoefu wa migogoro. Migogoro kidogo tu iliyopo wamepoteana na bado wameandaa migogoro mingi ya uchaguzi wa ndani ya chama.
Imetolewa na sisi:  
Majina ya wanaohama toka CHADEMA kuingia NCCR - MAGEUZI.

MFADHILI WA CHADEMA MBEYA AHAMIA NCCR-MAGEUZI.......

Mmoja wa kada Chadema, Emanuel Mwangoka (Cash Money), ambaye inadaiwa kuwa ndiye alikuwa mfadhili Mkuu wa mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Chadema), akikabidhiwa kadi ya chama kipya, alisema atatumia uwezo wake wote kama alivyofanya kwa sugu kuhakikisha NCCR-Mageuzi inaibuka na kung’ara mkoani 
 Mjumbe wa Halmshauri Kuu taifa ya chama hicho, Juju Danda, katika tukio la kuwapokea wanachama wapya 21 waliojunga na chama hicho, wakitokea Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

 Aliyekuwa Katibu wa Chadema Mkoa wa Mbeya na kujiunga na NCCR-Mageuzi , Januari 20 mwaka huu Eddo Makatta Mwamalala.


RAIS KIKWETE AZINDUA UJENZI WA UWANJA WA NDEGE WA KIGOMA

jk1 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wananchi wa Kigoma wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma leo Januari 4, 2013
jk2 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na viongozi wengine akikata utepe kuzindua  ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma leo Januari 4, 2013 
jk3 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wananchi wa Kigoma wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma leo Januari 4, 2013
jk4 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkurugenzi mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Uganda na Burundi Bw Phillipe Dongier, wakifunua kitambaa cha jiwe la msingi katika uzinduzi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma leo Januari 4, 2013
jk5
jk7Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na viongozi wengine baada ya uzinduzi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma leo Januari 4, 2013
jk8 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi mbalimbali wakipata maelezo juu ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa Kigoma toka kwa mhandisi George Sambaliwakati wa uzinduzi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma leo Januari 4, 2013
jk9 
Msanii Diamond na kundi lake wakitumbuiza wakati wa sherehe za  uzinduzi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma leo Januari 4, 2013
jk10Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Uganda na Burundi Bw. Phillipe Dongier akitoa hotuba kwa kiswahili fasaha wakati wa sherehe za  uzinduzi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma leo Januari 4, 2013
jo1 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Muungano eneo la Kibaoni wilayani Uvinza, Kigoma, akiwa njiani kuelekea mjini Kigoma, akitokea kukagua ujenzi wa daraja la Mto Malagarasi leo

KIKAO KAZI CHA MAAFISA HABARI WA SERIKALI CHAANZA MJINI DODOMA.

Picha na 1 
Waziri wa Habari, Vijana ,UtamaduninaMichezoDkt. Fenella Mukangara akifungua mkutano wa maafisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa serikali mjini Dodoma. Pamoja na mambo mengine amewataka kufanya kazi   kwa kuzingatia weledi na kutoa taarifa sahihi kwa umma mara kwa mara kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na serikali.
(PICHA NA ARON MSIGWA WA MAELEZO)
Picha na 2 
Maafisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Serikali wakiwa katika picha ya pamoja naWaziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo mara baada ya ufunguzi wa kikao kazi hicho  mjini Dodoma.
Picha na 3 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akizungumza na Maafisa Mawasiliano wa Serikali wakati wa Kikao kazi hicho mjini Dodoma.
Picha na 4Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene akiwasilisha mada kuhusu Mtazamo mpya wa Mawasiliano katika Vitengo vya Mawasiliano Serikalini wakati wa kikao kazi cha Maafisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Serikali mjini Dodoma.
Picha na 5 
Afisa Habari wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali  Sarah Reuben akichangia moja ya mada katika kikao kazi cha Maafisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Serikali mjini Dodoma.
Picha na 7 
Maafisa Mawasiliano wa Serikali wakiendelea na kikao kazi chao kujadili masuala mbalimbali ya utendaji kazi Mjini Dodoma.
Picha no 6 
Maafisa Mawasiliano wa Serikali wakiendelea na kikao kazi chao kujadili masuala mbalimbali ya utendaji kazi Mjini Dodoma.
Picha no 8 
Mmiliki na muendeshaji wa mtandao wahabari na matukio wa Mjengwa Blog kutoka Iringa Bw. Majjid Mjengwa akitoa mada kwa maafisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa serikali kuhusu Faida na Changamoto za matumizi ya mitandao ya kijamii kwa mawasiliano  serikalini mjini Dodoma.

CCM KYELA WASHTUKIA NJAMA ZA CHADEMA KUPANGA VURUGU KYELA WAKIDAI MAFUTA


NA MWANDISHI WETU,MBEYA. 
 
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), wilayani Kyela kimesema viongozi wa CHADEMA wanataka kutumia fursa ya uwepo wa mafuta katika tarafa ya Ntebela, kuwachochea wananchi kufanya fujo.

Kufuatia hilo,kiimewatoa hofu wananchi kipo makini, na kitahakikisha kinatoa elimu sahihi kwa wananchi juu ya utafiti wa mafuta uliofanyika hivi karibuni, na kubaini uwepo wa mafuta katika baadhi ya kata za tarafa hiyo.
Kaimu Katibu wa CCM wilayani humo, Richard Kilumbo, aliyasema hayo mbele ya Mjumbe wa halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), ya CCM, Sambwee Shitambala, kwenye maadhimisho ya miaka 36 ya CCM.

Kilumbo alisema:”Juzi na jana wenzetu wa CHADEMA wamekuwa wakiwashawishi wananchi ili tuingie kwenye vurugu kama ilivyotokea hivi karibuni mkoani Mtwara, baada ya kuonekana wilaya yetu inayo mafuta na utafiti umefanyika bado taarifa rasmi kutolewa”.

Aliongeza hivyo CHADEMA wanataka kutumia fursa hiyo ya kuwepo mafuta wilayani Kyela, kuwahamasisha wananchi kufanya vurugu ili machafuko yatokee wilayani humo kitendo ambacho Chama hakiwezi kukubali.

Kaimu Katibu wa CCM wilaya, aliwataka wananchi kuondoa hofu juu ya hilo, kwani mwananchi yeyote ambaye eneo lake analolimiliki likionekana kuwa mkondo huo wa mafuta atalipwa fidia stahili.

Kilumbo alisema wananchi waondoe dhana potofu inayopandikizwa na viongozi wa CHADEMA, kwani CCM itahakikisha hakuna mwananchi anayestahili haki yake halafu akadhurumiwa.

Aliongeza Chama kipo tayari kupambana na CHADEMA na vyama vingine vya upinzani wilayani humo, ambavyo vinajiandaa kufanya kama yale yaliyotokea mkoani Mtwara wananchi kugomea gesi isisafrishwe kwenda Dar es Salaam.

Kilumbo alisema:”Chama kitapita kata zote ambazo mkondo huo wa mafuta umeonekana na kutoa elimu sahihi juu ya uwepo wa mafuta wilayani kwetu…walifanikiwa kuwachochea wananchi wa Mtwara, lakini kwa wilaya ya Kyela wasahau kwani hilo halitawezekana kamwe”.

                  

No comments: