Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha
Mapinduzi Dk. Jakaya Kikwete akihutubia wananchi katika sherehe za miaka
36 ya CCM zilizofanyika jioni ya leo kwenye uwanja wa Lake Tanganyika
Mkoani Kigoma na kuhudhuriwa na wananchi mbalimbali waliojitokeza
kushiriki katika sherehe hizo.
Wawakilishi wa vyama rafiki vya
CCM kutoka nchini Burundi CNDD kinachotawala nchini humo, na PPRD
kinachotawala nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana akizungumza katika maadhimisho hayo.
Waziri
wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe akizungumzia mikakati ya Serikali
katika maadhimisho hayo juu ya urejeshaji wa huduma za treni katika
kituo cha Reli ya Kati cha Kigoma.
Kikundi cha ngoma kutoka nchini Burundi kikitumuiza katika maadhimisho hayo yaliyofanyika leo kwenye uwanja wa Lake Tanganyika.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Itikadi na Uenezi Nape Nnauye
akizungumza katika maadhimisho hayo katika uwanja wa Lake Taganyika.
Rais Jakaya Kikwete akiangalia picha zilizochorwa zikimuonesha yeye na
Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere wakati alipotembelea
mabanda ya maonyesho katika maadhimisho ya miaka 36 ya CCM
Rais Jakaya Kikwete akiangalia ndizi zinazozalishwa mkoani Kigoma katika banda la wakulima wa ndizi kutoka mkoa huo.
Rais
Jakaya Kikwete akiwapungia mkono wananchi wa mkoa wa Kigoma
waliojitokeza kwenye maadhimisho ya miaka 36 ya CCM kwenye uwanja wa
Lake Tanganyika.
Wananchi mbalimbali wakiwa wamejitokeza kwenye uwanja wa Lake Tanganyika.
Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Itikadi na Uenezi Nape Nnauye
akimtunza mmoja wa wasanii wadogo wa kikundi cha ngoma kutoka nchini
Burundi kilichoshiriki katika maadhimisho ya miaka 36 ya CCM.
Rais
Jakaya Kikwete akiangalia vikundi vya ngoma mara baada ya kuwasili
kwenye uwanja wa Lake Tanganyika kwa ajili ya kushiriki katika
maadhimisho ya miaka 36 ya Chama Cha Mapinduzi CCM Kutoka kushoto ni
Makamu Mweyekiti Bara Mzee Philip Mangula, Naibu Katibu Mkuu Bara
Mwigulu Nchemba na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana.
Wananchi wakiwa wamefurika kwenye uwanja wa Lake Tanganyika.
Vijana wa Chipukizi wa CCM wakipita kwa Gwaride la Heshima na Utii mbele ya Rais Jakaya Kikwete.
Vijana wa Chipukizi wakiimba wimbo wa Kwaya katika maadhimisho hayo.
Msanii Diamond akiongoza kundi lake katika kutoa burudani kwa wananchi waliojitokeza katika maadhimisho hayo.
Mwanamuziki
Diamond akiwaburudisha wananchi kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mkoani
Kigoma katika maadhimisho ya miaka 36 ya CCM mjini Kigoma leo.
 |
Madarasa ya shule ya
msingi kisa wilayani Rungwe yaliyokarabatiwa kwa ufadhili wa watu wa Jamhuri ya
Czech kupitia shirika la Without Mother (Tanzania) kwa kushirikiana na Bez Mamy
(Czech Republic)
|
 |
Mratibu wa miradi ya
Bez Mamy Africa na Mwenyekiti wa Without Mother Organization kulia Bw Chris
Zacharia akiwa na Vituko Issa Mkuu
wa shule ya msingi Simike Wilaya ya Mbarali wakijadili mpango wa kumalizia
jingo la darasa la awali ambalo wananchi walishindwa kulimaliza
|
 |
Without Mother
organization|Bez mamy wakiwa na Kamati ya maendeleo ya shule ya Msingi Ilenge
wilaya ya Rungwe baada ya mjadala wa kuifadhili shule hiyo kuboresha majengo na
kuiwekea umeme kwa ajili ya kuanzisha mafunzo ya computer shuleni hapo
|
 |
Mratibu wa Miradi ya
Bez Mamy Africa na Mwenyekiti wa Shirika la Without Mother Bw Chris Zacharia
akitambulishwa kwa wazazi na wanafunzi wa Shule ya Msingi Ilenge akiwa na
Mratibu wa miradi ya Shule wa Bez Mamy Eliška Nováková kushoto na mratibu wa
Elimu kata ya Kimo wilaya ya Rungwe
Bi Maulicia Mkusa kulia
|
 |
Darasa la chekechea
la shule ya msingi Galaula linalojengwa kwa ufadhili wa watu wa Jamhuri ya
Czech kupitia shirika la Without Mother (Tanzania) kwa kushirikiana na Bez Mamy
(Czech Republic)
Picha chini Mratibu wa Miradi za
Shule wa Shirika la Bez Mamy Eliška Nováková akikagua majengo ya nyumba za
waalimu katika shule ya Msingi Mahango wilaya ya Mbarali. Majengo hayo
yaliyokuwa yanajengwa kwa nguvu za wananchi wamesimama baada ya wananchi kukosa
uwezo wa kuyaendeleza
 |
Moses Mwasubira, ambaye alikuwa mwenezi wa Chadema wilaya ya Mbeya akikabidhiwa kadi ya NCCR na |
 |
Mmoja
wa kada Chadema, Emanuel Mwangoka (Cash Money), ambaye inadaiwa kuwa
ndiye alikuwa mfadhili Mkuu wa mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi
(Chadema), akikabidhiwa kadi ya chama kipya, alisema atatumia uwezo wake
wote kama alivyofanya kwa sugu kuhakikisha NCCR-Mageuzi inaibuka na
kung’ara mkoani |
Mjumbe wa Halmshauri Kuu taifa ya chama hicho, Juju Danda,
 |
Mjumbe
wa Halmshauri Kuu taifa ya chama hicho, Juju Danda, katika tukio la
kuwapokea wanachama wapya 21 waliojunga na chama hicho, wakitokea Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
|
 |
Aliyewahi
kuwa Katibu wa Chadema Mkoa wa Mbeya na kujiunga na NCCR-Mageuzi ,
Januari 20 mwaka huu Eddo Mwamalala, alisema wanachama hao waliomfuata
ni mtaji mkubwa wa kuhakikisha inakimaliza chadema mkoani hapa.
|




 |
CHAMA cha NCCR-Mageuzi,
kimesema taifa limepoteza muelekeo kutokana na viongozi wake wengi waliopewa
dhamana ya kuongoza kushindwa kutimiza wajibu wao, hali ambayo imesababisha
wananchi kuishi katika mkanganyiko mkubwa.
Hayo yalisemwa jana, Jijini hapa na
Mjumbe wa Halmshauri Kuu taifa ya chama hicho, Juju Danda, katika tukio la
kuwapokea wanachama wapya 21 waliojunga na chama hicho, wakitokea Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika
katika ukumbi wa hoteli ya Double J, mbele ya waandishi wa habari, Danda
alisema ili taifa liweze kupiga hatua za kimaendeleo ni lazima liwe na siasa
safi na uongozi bora.
Alisema kutokana na dhana hiyo kukosekana kwa viongozi
waliopewa dhamana ya kuongoza kumesababisha kuliacha taifa na wananchi wake
wakiishi katika mkanganyiko mkubwa unaotokana na kupanda kwa gharama za
maisha.
“Vyakula vimepanda, kadhalika nauli…. Kwa ujumla gharama za maisha
imepanda sana nahii yote imesababishwa na taifa kukosa watu wa kufanya siasa
safi ambazo zingetuletea viongozi bora” alifafanua Danda.
Alisema msingi pekee
wa taifa kupata maendeleo ni rasilimali watu ambayo imejengwa kwa kupewa elimu,
hivyo kitendo cha serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kukosa mitaala ya elimu
ni inaonesha taifa lilivyokosa muelekeo.
“Rasilimali watu ni muhimu katika
mchakjato wa maendeleo kuzidi hata hayo madini, lakini umeona kilichotokea juzi
pale bungeni…. Mwenyekiti wetu (Jems Mbatia-NCCRA-Mageuzi) alichokieleza na
kilichotokea”.
Aliongeza kuwa licha ya CCM iliyoiweka serikali madarakani
kujipambanua kwa itikadi ya ujamaa na kujitegemea, lakini serikali hiyo
imeshindwa kuisimamia hivyo kufanya taifa kushindwa kujitegemea na badala yake
limegeuka kuwa ombaomba.
Alisema hali hiyo inajidhihirisha kwenye bajeti ya
serikali, kwani zaidi ya asilimia 40 ya bajeti hiyo inategemea msaada wa wafadhili
jambo linalokinzana na mfumo wa itikadi yake iliyojiwekea kama malengo wakati
ikitafuta dhamana ya kupewa nafasi ya kuongoza nchi.
Kwa upande wake mwakilishi
wa kundi la wanachama 21 waliohamia ndani ya NCCR-MAgeuzi, Moses Mwasubira,
ambaye alikuwa mwenezi wa Chadema wilaya ya Mbeya Mjini, alisema wamefikia
uamuzi huo kutokana na sababu mbalimbali.
Miongoni mwa sababu hizo ni kudai
kuwa uongozi wa taifa wa Chadema kushindwa kujenga Demokrasia ya kweli ndani ya
chama kwa kukumbatia ufisadi wa kutumia vibaya ruzuku ya chama na kuwaacha wa
mikoani wakifanya kazi kubwa ya kuchangisha fedha.
Uongozi mbaya wa Katibu Mkuu
wa chama hicho taifa,Dk.Willbroad Slaa na Mwenyekiti wake Freeman Mbowe,
kushindwa kusimamia katiba ya chama hicho katika kutatua migogoro, badala yake
wakitumia na kuamini kuwa kufukuza wanachama tena kwa majungu ndio suluhisho la
kukijenga na kukiimarisha chama.
Lakini pia walilalamikia chama hicho kujaa
utashi wa nguvu ya umma na kulazimisha maandamano, migomo vitu ambavyo si vya
lazima na kwamba kamwe hiyo si njia sahihi na malengo ya kweli ya kutafuta
ukombozi.
Naye mmoja wa kada Chadema, Emanuel Mwangoka (Cash Money), ambaye
inadaiwa kuwa ndiye alikuwa mfadhili Mkuu wa mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph
Mbilinyi (Chadema), akikabidhiwa kadi ya chama kipya, alisema atatumia uwezo
wake wote kama alivyofanya kwa sugu kuhakikisha NCCR-Mageuzi inaibuka na
kung’ara mkoani hapa.
Kwa upande wake aliyewahi kuwa Katibu wa Chadema Mkoa wa
Mbeya na kujiunga na NCCR-Mageuzi , Januari 20 mwaka huu Eddo Mwamalala,
alisema wanachama hao waliomfuata ni mtaji mkubwa wa kuhakikisha inakimaliza
chadema mkoani hapa.
Na Moses Ng’wat, Picha na Mbeya yetu
|
|
No comments:
Post a Comment