Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman
Kinana akiwahutubia wananchi katika uwanja wa michezo wa Ilulu mjini
Lindi wakati akihitimisha ziara yake mkoani humo leo kabla ya kuendelea
na ziara mkoani Mtwara kesho. Kinana amesema viongozi wanatakiwa kuwa
waadilifu na wanaojituma kuwatumikia wananchi, akaongeza kwamba muda wa
kulindana haupo tena na kiongozi akiharibu awajibike mwenyewe kwa makosa
yake na ni muhimu kiongozi akiingia madarakani ajue na wakati wa
kutoka. Wakati huohuo Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi Nape
Nnauye amesema katika sakata la ESCROW kila mtu aliyehusika abebe
msalaba wake.Nape alisema CCM haijabadili msimamo wake ambapo alifafanua
kama katika sakata la Richmond Waziri Mkuu alijiuzulu , hivyo hata
kwenye ESCROW atakayebainika kuhusika naye achukuliwe hatua.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Mzee
Ali Mtopa akizungumza na wananchi katika mkutano huo wa hadharawakati
akimkaribisha Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na
Uenezi Nape Nnauye akinukuu baadhi ya vifungu vya katiba mpya
inayopendekea wakati alipokuwa akifafanua mambo mbalimbali kwa wananchi
kuhusu katiba hiyo
Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisisitiza jambo katika mkutano huo wa hadhara.
Umati wa wananchi ukiwa katika mkutano huo
Umati wa wananchi waliojitokeza katika mkutano huo ukisubiri kuanza kwa mkutano.
Baadhi ya vijana wa chuo cha VETA wakionyesha kadi zao za umoja wa Vijana wa CCM UVCCM katika mkutano huo.
Moja ya vikundi kikitumbuiza katika mkutano huo
wananchi wakifuatilia mkutano huo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwapungia mkono
wananchi mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ilulu mjini Lindi.
Nape Nnauye akiwasili katika mkutano huo.
Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akijumuika na wanachama wa CCM kutoka Tawi la Magogoni/Rahaleo
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwapa mafundi bati
wakati walipokuwa wakipaua jengo la umoja wa vikundi vya akina mama
washonaji nguo..
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia nyavu za
kuvulia samaki wakati alipokitembelea mradi wa kuvua samaki huko
Jamhuri Machole.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa munyumba ya mwalimu shule ya msingi Nanyenje mkoani Lindi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupalilia shamba la mihogo la kikundi cha kuzalisha mbegu bora za muhogo.
Muhogo wenyewe ndiyo huu.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuchimba mtari wa kilimo cha umwagiliaji mbogamboga Mingoyo Mnazi Mmjoa.
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili kwenye uwanja wa Ruangwa
Likangara tayari kuhutubia wakazi wa wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili kwenye uwanja wa Ruangwa
Likangara tayari kuhutubia wakazi wa wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.
Wananchi
wa Ruangwa wakionyesha furaha yao wakati wa kumkaribisha Katibu Mkuu wa
CCM kwenye uwanja wa mkutano Ruangwa Likangara.
No comments:
Post a Comment