Monday, November 24, 2014

WATU ZAIDI YA 25 WAJERUHIWA VIBAYA KATIKA AJALI YA COSTA SENJELE MBEYA AKIWEPO NA MWANDISHI WA HABARI KENNETH MWAZEMBE



Baadhi ya majeruhi wakitafuta mizigo yao mara baada ya kutoka ndani ya basi hilo


Baadhi ya majeruhi wakitoka ndani ya basi hilo







Baadhi ya abilia wakitaka kumpiga Dereva wagari ya aina ya Suzuki kuwa yeye ndio alisababisha ajali hiyo kwa kuyumbayumba kwake barabarani

Moja ya wasamaria wema akiwazuia abiria wenye hasira kali kutaka kumpiga mzee huyo Mwenye Suzuki ambae alijulikana kwa jina moja tu mzee Mtawa

Mwandishi wa habari Kenneth Mwazembe akiwasili katika Hospitali ya Ifisi akisindikizwa na  Joseph Mwaisango  wa Mbeya yetu baada ya kupata ajali eneo la Senjele wilayani Mbozi  akiwa anatokea shambani kwake  huko wilayani  Momba kwa taarifa za awali inasemekana amevunjika mguu wa kushoto




WATU zaidi ya 25 wajeruhiwa vibaya katika ajali iliyotokea jana baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Toyota Costa kutoka Mbozi kuelekea Mbeya kupinduka katika eneo la  Senjele wilayani Mbozi Mkoa wa Mbeya.
Ajali hiyo ilihusisha gari aina ya Costa lenye namba za usajili T 336 CJY ambalo lilipinduka baada ya kumshinda dereva wakati akijaribu kulikwepa gari linguine aina ya Suzuki lenye namba za usajili T 327 ARZ.
Kwa mujibu wa baadhi ya majeruhi walionusurika kwenye ajali hiyo walisema chanzo ni dereva kushindwa kulimudu gari la abiria baada ya kulikwepa gari dogo kutokana na kuwa na mwendokasi pamoja na mvua kubwa iliyokuwa ikiendelea kunyesha.
Baadhi ya majeruhi walikimbizwa katika Hospitali teule ya Ifisi na wengine wakipelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya kwa ajili ya matibabu zaidi.
Mwisho.
Picha na Mbeya yetu

No comments: