Kituo
cha Kisasa cha Uchunguzi na Matibabu ya magonjwa ya binadamu
kinachojengwa katika Chuo Kikuuu cha Dodoma UDOMT kikiwa katika hatua
za mwisho mwisho za ukamilishwaji, Kituo hiki kitahudumia wagonjwa
kutoka maeneo mbalimbali ya mikoa ya jirani ya na mkoa wa Dodoma na
kinajengwa kwa ufadhili wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF kwa
gharama ya shilingi Bilioni 36 ambazo zimetolewa na mfuko huo kwa
silimia 100, Akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali wanaohudhuria
kongamano la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya linalofanyika kwenye hoteli
ya Dodoma mjini humo walipotembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa
kituo hicho, Kaimu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Mlacha Shaaban amesema
“Kituo hiki kitajikita zaidi kwenye magonjwa ya uchunguzi na utafiti
pia kitatoa wataalamu kutoka katika kitivo cha afya cha Chuo kikuu cha
UDOM na wataalamu watakaofanya kazi katika kituo hicho watakuwa
wakiffundisha wanafunzi na kuhudumia katika kituo hicho,Kituo hicho
kinatarajiwa kuanza kutoa huduma ifikapo Januari 2015
Baadhi
ya waandishi wa habari wakiingia katika jengo la kituo cha Utafiti na
tiba cha UDOM kinachojengwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF.
Kaimu
Makamu Mkuu wa chuo Kikuu cha UDOM Profesa Mlacha Shaaban akizungumza
na wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali walipotembelea ujenzi wa
kituo cha Tiba na Utafiti kinachojengwa katika chuo kikuu cha UDOM.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bw. Raphael Mwamoto akizungumza na waandishi wa habari kwenye kituo hicho
Waandishi wa habari wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bw. Raphael Mwamoto akimsikiliza Athman Rehani Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii CHF
Mshauri
Mtaalam wa Mradi huo wa ujenzi wa kituo kutoka kampuni ya Hab Consult
Bwana Habib Nuru akiwatembeza waandishi wa habari katika jengo hilo.
Mshauri
Mtaalam wa Mradi huo wa ujenzi wa kituo kutoka kampuni ya Hab Consult
Bwana Habib Nuru akitoa maelezo kwa waandishi wa habari wakati
walipokuwa wakitembelea kituo hicho kulia kwake ni Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bw. Raphael Mwamoto
Mganga Mkuu wa mkoa wa Singida Dr. Doroth Gwajima akitoa mada katika kongamano hilo linalofanyika mjini Dodoma kwa siku mbili.
Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari na waandishi wa habari wakiwa katika kongamano hilo.
Mwanaamani
Mtoa Katibu wa Mkuu wa mkoa wa Tanga akiwaonyesha kitu Mkuu wa Mkoa wa
Tanga Chiku Galawa kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya
Taifa ya Afya NHIF Khamis Mdee.
Grace Michael mmoja wa maafisa wa NHIF akifuatilia jambo wakati mkutano huo ukiendelea.
Baadhi ya waandishi wakiwa katika mkutano huo.
Meneja
wa Masoko wa NHIF Angela Mziray akisikiliza jambo wakati alipokuwa
akiongea na Grace Mchaele mmoja wa maofisa wa mfuko huo.
No comments:
Post a Comment