NYARAKA ZA MRADI WA MAJI MASOKOPIPED WARER SUPPLY SYSTEM AND CIVIL WORKS LGA/071/RDC/2009/10/38 |
MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA RUNGWE VERONIKA KESSY |
MOJA YA MIRADI YA MAJI RUNGWE |
Na Ibrahim
Yassin,Rungwe
HALMASHAURI wilayani
Rungwe Mbeya huenda ikafirisiwa mali zake baada ya madiwani katika Halmashauri
hiyo kupinga ushauri wa mwanasheria wa kutaka kuwalipa wakandarasi wawili fedha
za mradi wa maji uliopo kata ya masoko.
Mradi huo wa masoko ni
moja wapo ya miradi ya kimkakati ambayo ilianza kutekelezwa mwaka 2009/2010
ambapo bajeti ya mradi huo ni Bil,4.7 ambapo mkandarasi aliyepewa tenda hiyo ni
Luck na Osaka Contruction Compan LTD.
Mradi huo uliotengewa
kiasi cha Tshs,4,754,420 mpaka kukamilika kwake ambapo mkataba ulisainiwa tarehe 25/5/2010 kati ya
Halmashauri ya wilaya hiyo na wakandarasi hao kwa kipindi cha miezi 18.
Mpaka hivi sasa kazin
ilyofanyika ni ya kiasi cha Tshs,1.7 Bilioni na kiasa alicholipwa mkandarasi ni
Tshs,1.2 Bilioni ambapo taarifa hiyo ipo katika hotuba ya waziri wa maji ya
mwaka 2014/2015.
Hata hivyo mradi huu
uliingia dosari kati ya muajiri na mkandarasi hadi kufikia muajiri kutomlipa
mkandarasi satifiketi namba 3 na 4 ambapo mkandarasi huyo alipeleka shauri hilo
kwa msuruhishi wa Baraza la ujenzi wa Taifa kwa ufumbuzi zaidi.
Katika shauri hilo
mkandarasi alishinda kesi hiyo na kutakiwa kulipwa zaidi ya milioni mia saba
ndani ya wiki tatu ambazo zinamalizika kesho na kupelekea kuitishwa kikao kikao
cha dharula cha baraza la madiwani kujadili suala la kulipa au kukata rufaa.
Mwenyekiti wa
Halmashauri hiyo Wilfred Mwakisangula alipofungua kikao alitaja kuwa na ajenda
moja ya kujadili suala la mradi huo ambapo madiwani walipitisha hoja ya kumtaka
mwanasheria kukata rufaa bila kujali athari zinazoweza kujitokeza.
Mwanasheria katika
halmashauri hiyo Merik Luvanga aliliambia baraza hilo kuwa iwapo watakata rufaa
kunauwezekano wa kushindwa kesi hiyo kwa kuwa baadhi ya nyaraka hazionekani na
kuwa kunauwezekano halmashauri ikalipa fedha zaidi kama fidia kwa mkandarasi
huyo.
Mwisho..
No comments:
Post a Comment