NI NGUMU KUAMINI LEO LAKINI MUNGU NDIO KAAMUA HILI LITOKEE BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA NA LIHIMIDIWE |
AMINA MWASEBA AKIWA NA MUMEWE SIKU YA SHEREHE YA KUMUAGA MJINI SUMBAWANGA KABLA YA NDOA YAO ILIYOFANYIKA 26.07.2014. |
AMINA AKIWA NA MUMEWE KATIKA SAFARI YAO WAKIELEKEA DSM KWA HAFLA YA KUWAPONGEZA WAFANYAKAZI BORA WA FAIDIKA AKIWEMO NA AMINI MWASEBA AKIWA MFANYAKAZI BORA WA MWAKA 2014 NA MUMEWE AKIWA NI KIONGOZI WA FAIDIKA MKOA WA KIGOMA
Huzuni na majonzi imetanda leo katika mji wa kahama baada ya bus la
Wibonela Express linalofanya safari zake Kahama -Dar kupinduka baada ya
kutoka stand kuu ya kahama km chache toka stand katika eneo la Phantom
na kuua watu wanne.
Kwa taarifa za awali chanzo chz ajali hiyo ni mwendo kasi kufuatilia taarifa zetu.
Wakazi wa Kahama wakiwa eneo la ajali leo asubuhi
Chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi kuendesha mwendokasi wakati akitoka katika
kituo kikuu cha mabasi mjini Kahama na alipofika kwenye kona ya kutoka mjini
Kahama kuelekea Isaka basi lilimshinda huku
yeye akiruka kutoka kwenye gari na kuangukia katika mtaro na basi kupinduka.
Mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Kahama Dkt
Joseph Ngowi amesema watu waliopoteza maisha katika ajali ya basi leo asubuhi
mjini Kahama ni wanne ambao ni Amina Emmanuel ambaye alikuwa mjamzito mkazi wa
Kigoma, Salum (amefahamika kwa jina moja)
mtoto wa miezi mitatu Robin Jordan na mwanamme mmoja ambaye jina lake
halikufahamika mara moja huku majeruhi wakiwa 41.
Tukio hilo limetokea leo saa 12 asubuhi katika
eneo la Phantom kilomita chache kutoka Stand ya Mabasi mjini Kahama baada ya basi aina ya Scania lenye namba za usajili T
412 CGN mali ya Wibonela Ambalo lilikuwa likitokea mjini Kahama kwenda jijini
Dar es Salaam kuacha njia na kupinduka.
Mganga
mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Kahama Dkt Joseph Ngowi amewataja waliojeruhiwa katika ajali hiyo kuwa
ni Maulid Shaban (44) mkazi wa Ushirombo, Athuman Issa (21) mkazi wa Kahama,
Jordan Mbeya (28) mkazi wa Kasulu, Brandina Patrick (24) mkazi wa Kasulu, Oscar
Lameck (19) Mkazi wa Kigoma, Stamili Shaban (38) mkazi wa Dodoma, Neema Dastan
(18) Mkazi wa Kahama na Monica Gadson (35) mkazi wa Kahama.
Majeruhi
wengine ni Nickson Andati ambaye ni Mchungaji mkazi wa nchi ya Rwanda (34)
Lucas Mlezi (48), Joyce Fred (28) Asnati Remtula (27) , Eveline Hamis (6),
Happy Hamis (30), Japhet Masha (29), Jackson Elisanto (26), Buligelila Ramadhani
(40) na Rita Bryson (25) wote wakazi wa Kahama.
Pia
kuna Irene Wilson (17) mkazi wa Kasulu, John Lembo(45) Mkazi wa Bariadi, Hamis
Shaban (31) mkazi wa Kahama, Emmanuel Lambambo (32) mkazi wa Kigoma, Kashindye
Masanja (28), Frenk Kishimba (21) Peter Bahati (22) wote wakazi wa Kahama,
Iseme Ilila (36) mkazi wa Katoro Geita, Ebrania Saga (30) mkazi wa Kigoma, na
Anika Amdani (35) Mkazi wa Kahama.
Wengine
ni Shaban Omary (16) ambaye ni mkazi wa Dodoma,Grolia Moses (18) mkazi wa
Kahama, Agnes Broto (35) Mkazi wa Ngara, Kulwa Said (40) mkazi wa Kahama, Peter
David (42) mkazi wa Kahama,Tunga Lazaro (22) mkazi wa Mariadi, na Happy David
(32) huku majeruhi wengine wakishindwakutambulika kutokana na kuwa mahututi.
Miili
ya marehemu ipo kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya
wilaya ya Kahama na majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu
Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga
limethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
No comments:
Post a Comment