Kaimu Afisa
Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, Christopher Nyambaza,
akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo wakati akifunga
mafunzo ya wiki moja ya Wasaidizi wa kisheria yaliyotolewa na House of
Peace.
kaimu Mwanasheria
wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, Amon Nyingi, akimkaribisha mgeni
rasmi katika kufunga mafunzo ya wasaidizi wa kisheria.
Mratibu wa Mafunzo ya Wasaidizi wa Kisheria, Dorothy Ndazi kutoka House of Peace akisoma taarifa kwa mgeni rasmi.
Mmoja wa Wanafunzi wa mafunzo ya wasaidizi wa Kisheria, Japhety Mushumba akisoma risala kwa niaba ya wanafunzi wenzie.
Mmoja
wa Wanafunzi wa mafunzo ya wasaidizi wa Kisheria, Japhety Mushumba
akikabidhi risala kwa niaba ya wanafunzi wenzie kwa mgeni rasmi.
Washiriki wa Mafunzo hayo.
Picha ya pamoja.
KUTOKUJUA
maswala ya kisheria kwa Wazee wa Mabaraza ya Kata kunachangia migogoro
mingi katika jamii na kupelekea kuwa na mlundikano wa kesi mahakamani
jambo ambalo lilipaswa kumalizwa kwenye mabaraza hayo, imebainishwa.
Hayo
yalibainishwa mwishoni mwa wiki na Afisa utumishiwa Halmashauri ya
Wilaya ya Rungwe, Christopher Nyambaza, alipokuwa akifunga mafunzo ya
wiki moja ya wasaidizi wa kisheria kwa niaba ya Mkurugenzi ya
Halmashauri hiyo yaliyotolewa na Shirika la House of Peace mafunzo
yaliyofanyika katika ukumbi wa DM Motel Tukuyu mjini.
Nyambaza
alisema Halmashauri itaangalia uwezekano wa kuwaingiza kwenye mabaraza
ya kata ya Ushauri vijana waliopitia mafunzo ya Usaidizi wa Kisheria ili
kupunguza migogoro isiyokuwa na sababu kutokana na madai yao
kupindishwa kwa kutokuwa na ufahamu wa kisheria kwa Wazee wa Mabaraza.
Alisema
kawaida Wazee wa mabaraza ya Kata huchaguliwa kutokana na umaarufu
walionao kijiji lakini wanakuwa hawaelewi maswala ya kisheria jambo
ambalo linasababisha baadhi ya maamuzi wanayotoa kutokuwa na uwiano
mzuri wala kusaidia kutatua migogoro katika jamii hususani migogoro ya
ardhi na ndoa.
Awali
akitoa taarifa ya mafunzo hayo, Afisa Sheria na Mratibu wa Mafunzo wa
House of Peace, Dorothy Ndazi,alisema hiyo ni taasisi isiyokuwa ya
kiserikali inayofanya kazi ya kuhamasisha jamii juu ya haki za wanawake
na watoto, Ndoa, pia kushawishi na kuleta sheria na sera zinazothamini
haki na hadhiya wanawake na watoto ikiwa ni pamoja na kutoa ushauri
nasaha kwa waathirika wa unyanyasaji na wale wanaonyanyasa.
Ndazi
alisema katika kutekeleza majukumu yake katika jamii Shirika limetoa
mafunzo kwa wanafunzi 25 yaliyoanza Oktoba 28 hadi Novemba 28 mwaka huu
ambao wamefundishwa Elimu ya Kisheria( Paralegal training) ambapo
wamepata mafunzo kwa ujumla kuhusu sheria za ndoa, ardhi,ukatili wa
kijinsia,haki za kibinadamu,sheria za ajira, makosa ya kujamiiana,
utatuzi wa migogoro na kanuni za maadili, miiko na uwajibikaji wa
wasaidizi wa kisheria.
Alisema mafunzo hayo yamewanufaisha wanakijiji husika kutoka kata 25 za Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe ambazo
ni Msasani, Bgamoyo,Bulyaga, Kawetele,
Mkandana,Kyimo,Malindo,Kiwira,Mpuguso na Ilima ambao wanaweza kuwa
msaada katika jamii zao.
Kwa
upande wake Wananfunzi waliohitimu Mafunzo hayo katika Risala yao kwa
mgeni rasmi iliyosomwa na Japhet Mushumba, walitoa ombi kwa Halmashauri
kuwasaidia wahitimu hao ili waweze kutambulika na viongozi wa Kata na
Vijiji pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama, ambapo walisema
kutambulika kama wasaidizi wa kisheria katika jamii kutaweza kuleta
ustawi na kuongeza amani na upendo.
NA MATINYA MBEYA
No comments:
Post a Comment