Mkurugenzi
Mtendaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini Tanzania TCRA Profesa John
Nkoma akizungumza katika mkutano na Mablogger wakati alipofungua mkutano
huo uliojadili jinsi ya kuripoti kwa usawa habari za uchaguzi wa
serikali za mitaa, Ubunge na Rais kuanzia mwaka huu mpaka mwakani,
Mkutano huo umefanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es
salaam ambapo pia viongozi wa Muda wa kuratibu uanzishwaji wa Chama cha
Mablogger wamechaguliwa ambao ni Joachim Mushi, Aron Msigwa mwakilishi
kutoka serikalini, Shamimu Mwasha Blog za Biashara, Francis Godwin
mablogger wa mikoani, Othman Maulid mwakilishi kutoka Zanzibar, Khadija
Khalili, William Malecela na Henry Mdimu ambao wataongoza kwa muda
wakati wa mchakato huo mkutano huo umesimamiwa na Mamlaka ya Mawasiliano
TCRAMkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Assah Mwambene akifunga rasmi mkutano huo uliofanyika Mlimani City jijini Dar es salaam.
Kutoka
kushoto ni Josephat Lukaza wa Lukaza Blog, Shamimu Mwasha wa
8020Fashion na Geofrey Wapamoja Blog wakiwa katika mkutano huo
Baadhi maofisa wa TCRAwakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika mkutano . Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini Tanzania TCRA Profesa John Nkoma katikati
Mkurugenzi wa Utangazaji TCRA Habbi Gunze ma Aron Msigwa Ofisa
Mwandamizi kutoka Idara ya Habari Maelezo wakiwa katika mkutano huo.
Andrew Kisaka Ofisa Mwanamizi wa Utangazaji TCRA akitoa mada katikamkutano huo.
No comments:
Post a Comment