Saturday, November 1, 2014

KIVUKO KIPYA CHA MSANGAMKUU CHAWASILI MKOANI MTWARA

Kivuko cha Msangamkuu( MV Mafanikio) chenye uwezo wa kubeba uzito wa tani 50 pamoja na abiria 100 kikiwasili Mkoani Mtwara tayari kwa kuanza kazi rasmi ya kutoa huduma kati ya upande wa Mtwara Mjini na Msangamkuu.

Kivuko kipya cha (MV Mafanikio) kama kinavyoonekana mara baada ya Serikali kutekeleza ahadi yake ya kuwaletea wananchi wa Mtwara Kivuko hicho kipya.

Wananchi wakikimbia kuingia ndani ya Kivuko hicho kipya cha (MV Mafanikio) huku wakishangilia kuonyesha furaha yao mara baada ya kivuko hicho kuwasili mkoani Mtwara.(P.T)

Baadhi ya kina mama nao walipata fursa ya kukaa na kufurahia ndani ya kivuko hicho kipya.

Usafiri huu wa Mitumbwi ndio uliokuwa unategemewa na wananchi hao wa Mtwara kabla ya ujio wa Kivuko kipya cha Msangamkuu.

Mkurugenzi wa Ufundi na Umeme (DTES) Dkt. Wiliam Nshama kutoka Wizara ya Ujenzi akipita kukagua Kivuko hicho kipya cha Mv Mafanikio. Picha zote kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Ujenzi.

No comments: