Klabu ya
Mbeya City Council Football Club leo 25/11/2014 inatoa ufafanuzi wa
mbalimbali ikiwemo suala la utaratibu wa maslahi kwa watumishi wake
(benchi la ufundi, wachezaji na watumishi wengine) na uwepo wa fedha za
wadhamini katika klabu yetu.
Uamuzi wa
kutoa taarifa hii umefikiwa baada ya vikao vya menejimenti na kamati ya
fedha na utawala kufuatia taarifa mbalimbali zinazozalishwa kila siku
juu ya klabu yetu toka katika vyanzo ambavyo sio vya klabu.
MASLAHI YA WACHEZAJI
Hivi
karibuni baadhi ya wadau wa mchezo wa mpira wa miguu wamehusisha matokeo
ya uwanjani iliyopata timu na maslahi kwa wafanyakazi wa klabu kama
taasisi.
Sehemu kubwa ya wafanyakazi wa klabu ikijumuisha timu ni wafanyakazi chini ya masharti ya mkataba chini ya muajili ambaye ni Halmashauri ya jiji la Mbeya, Hivyo maslahi ya mfanyakazi(kwa kada hii) hujadiliwa na kukubaliana kwa pande zote mbili(Klabu kwa niaba ya muajiri na Mchezaji kama muajiriwa) kulingana na bei ya soko ndipo mkataba husainiwa

Klabu
imeweka utaratibu wa namna ya wafanyakazi wake kujadiliana na mwajili
kuhusu mambo mbali mbali yenye lengo la kuboresha utendaji wa kazi na
mazao yake pamoja na masuala ya maslahi pindi kukiwa na haja hiyo.
Mishahara
ya wachezaji pamoja na kuamuliwa kwa makubaliano baada ya majadiliano
ya pande zote mbili pia bei ya soko huangaliwa na kuzingatiwa. Msimu wa
2014/2015 mishahara ya wachezaji ilipanda kati ya asilimia 100 – 300(%)
ikilinganishwa na msimu uliopita 2013/2014.
Posho zote zitolewazo na klabu zilirekebishwa ikilinganishwa na msimu uliopita kwa kuzingatia makubaliano kati ya wachezaji na menejimenti kabla ya kuanza kwa msimu huu.
Klabu
inatambua wazi kuwa mpira ni ajira kama zilivyo ajira zingine,maslahi
haya yamewekwa kwa makusudi ili kuboresha hali za maisha za wafanyakazi
wetu hasa wachezaji kwani hiyo ndiyo ajira yao.
Ukiondoa mshahara unaoendelea kulipwa kila mwezi hakuna mfanyakazi yeyote anayedai chochote kati ya maslahi yake.
Ukiondoa mshahara unaoendelea kulipwa kila mwezi hakuna mfanyakazi yeyote anayedai chochote kati ya maslahi yake.
FEDHA ZA WADHAMINI:
Pamoja na kuwa na kipengele cha kutotoa siri (Confidentiality)za mikataba yetu na wadhamini wetu, klabu inasikitishwa namna ambavyo umma wa wanamichezo unavyopotoshwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa changamoto ambazo klabu inapitia hivi sasa kama taasisi zinatokana na kuwepo kwa fedha za wadhamini.

inaomba ikumbukwe kuwa katika msimu uliopita 2013/2014 ilitumia zaidi ya
shilingi milioni 700 kutoka katika vyanzo vya mapato ya ndani ya
Halmashauri ikiwa kama mmiliki wa klabu. Wadhamini kwa mujibu wa
makubaliano hawajatoa wala hawatoi fedha zote mara moja kwa mujibu wa
mkataba, fedha hizo hutolewa kila mwezi na kwa awamu.
Matumizi
ya kawaida ya klabu kwa mwezi si chini ya shilingi 49,000,000.00(bila
kuhusisha mishahara), katika kipindi cha Julai-Sept 2014, Klabu ilikuwa
na mdhamini mmoja tu ambaye ni Binslum tyres Co Ltd anayetoa shilingi
15,000,000.00 kwa mwezi sawa na shilingi 180,000,000.00 kwa mwaka kwa
mujibu wa mkataba uliopo.
Ukiangalia
mahitaji ya klabu kwa mwezi mmoja hapo juu, fedha hizi za mdhamini
zilichangia asilimia 30.6(%) ya gharama za klabu kwa mwezi. Hii ikiwa na
maana kuwa bado asilimia 69.4(%) ya gharama za uendeshaji wa timu
zilitoka Halmashauri.
Kuanzia
mwezi oktoba 2014 ambapo kampuni ya coca cola ilisaini mkataba wa
udhamini na klabu yetu. Kampuni ya Coca Cola itakuwa inatoa fedha
taslimu Tsh 60 milioni ambazo inazitoa kwa mwaka. Fedha hizi hutolewa
kila baada ya robo mwaka shilingi milioni 15. Hii ina maana kuwa coca
cola inatoa shilingi 5,000,000.00 milioni kila mwezi.
Hivyo
kuanzia mwezi oktoba klabu inapata toka kwa wadhamini wake wawili
(Binslum Tyre Co Ltd na Coca Cola Kwanza) shilingi 20,000,000.00 kwa
mwezi. Fedha hizi zinachangia asilimia 40.8(%) ya gharama za uendeshaji
wa timu kwa mwezi na asilimia 59.2(%) ya gharama hizo bado zinabebwa na
Halmashauri.
Uwepo wa wadhamini hivi sasa haujaongeza fedha kutoka katika bajeti hiyo bali umepunguza utegemezi wa timu kwa Halmashauri.
Uwepo wa wadhamini hivi sasa haujaongeza fedha kutoka katika bajeti hiyo bali umepunguza utegemezi wa timu kwa Halmashauri.
Hivyo
basi shutuma zinazotolewa na baadhi ya wadau kuwa changamoto ambazo timu
inazipitia kwa sasa ni kutokana na kuwepo kwa fedha za wadhamini ni
UPOTOSHAJI MKUBWA.
MWALIMU JUMA MWAMBUSI
Mwalimu Juma Mwambusi ni muajiriwa wa Halmashauri ya jiji la Mbeya anayesimamia benchi la ufundi la timu yetu.
Mwalimu Juma Mwambusi ni muajiriwa wa Halmashauri ya jiji la Mbeya anayesimamia benchi la ufundi la timu yetu.
Menejiment
ilikutana na Mwl Juma Mwambusi katika vikao vyake vya kawaida kupitia
changamoto kadhaa zilizojitokeza katika michezo saba ya awali mara baada
ya kuwasilisha ripoti ya maendeleo ya timu. Mwalimu Mwambusi na
menejiment tumeridhiana kwa faida ya mpira wa miguu na jamii
inayoizunguka timu yetu anaendelea kuifundisha timu ya Mbeya City Fc.
Nachukua
nafasi hii kuujulisha umma kuwa Mwl.Juma Mwambusi ndiye Kocha Mkuu wa
timu na hivi sasa anandaa program ya mafunzo kwa mzunguko wa pili wa
ligi unaotarajia kuanza disemba 2014.
MWISHO
Klabu
kama taasisi inayokuwa inapitia katika changamoto mbalimbali, ni imani
ya menejimenti kuwa changamoto hizi zitaiimarisha na kuikomaza klabu ili
kuwa klabu bora zaidi kwa vizazi vijavyo.
Tunatoa shukrani za dhati kwa wadau wetu wote wanaoendelea kutuunga mkono katika kipindi hiki.
Imetolewa na
Tunatoa shukrani za dhati kwa wadau wetu wote wanaoendelea kutuunga mkono katika kipindi hiki.
Imetolewa na
E.E.Kimbe
KATIBU MKUU
MCC FC
KATIBU MKUU
MCC FC
No comments:
Post a Comment