Watanzania wanatakiwa kupigia kura
jezi ya timu ya Taifa ya nyumbani na ugenini kupitia mtandao wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wa www.tff.or.tz ambapo jezi hizo zimewekwa.
TFF ilipokea mapendekezo ya
mwonekano mpya wa jezi ya timu ya Taifa kutoka kwa Watanzania 86. Jezi
11 za nyumbani, bukta nane za nyumbani, jezi nane za ugenini na bukta
tano za ugenini ndizo zimepitishwa kwa ajili ya kupigiwa kura.
Mwisho wa kupiga kura ni Desemba
31 mwaka huu. Mpigaji kura anatakiwa kubonyeza kwenye jezi na bukta
ambayo ameichagua. Anatakiwa kufanya hivyo kwa jezi ya nyumbani na jezi
ya ugenini.
Tunawashukuru wote waliojitokeza kupendekeza mwonekano mpya wa jezi ya timu ya Taifa.
No comments:
Post a Comment