Baada ya
Chelsea kupoteza mchezo kwenye ligi dhidi ya Newcastle jumamosi, Arsenal
kudhalilishwa na Stoke City, huku Man City na Liverpool wakishinda –
usiku wa kuamkia leo ilikuwa zamu ya Man United kucheza dhidi ya
Southmpton.
Matokeo
ya mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa St Mary umemalizika kwa United
kushinda mechi ya 5 mfululizo na kufanikiwa kushika na nafasi ya tatu
kwenye ligi, mara ya kwanza tangu Sir Alex Ferguson alipokuwa Kocha wao.
Magoli mawili ya Robin Van Persie yalitosha kuifanya United kuwaondoa West Ham katika nafasi ya 3.
Pelle aliifungia Southampton goli la Kufutia machozi kwenye mchezo huo
No comments:
Post a Comment