Kimbunga kikali kwa Jina Irma kimesababisha uharibifu mkubwa katika eneo la Caribbean ambapo takriban watu saba wameuawa.
Kisiwa kidogo cha Barbuda kilisemekana kukumbwa na uharibifu mkubwa hadi kutajwa kuwa kisichoweza kukalika huku maafisa wakionya kuwa himaya ya Uingereza ya St Martin imeharibiwa kabisa.
Jitihada za uokoaji zinatatizwa kutokana na kuwepo ugumu wa kuyafikia maene mengine.
Wakati huo huo upepo umetajwa kupata nguvu na kuwa vimbunga viwili.
Kimbunga Irma cha kiwango cha tano, ambacho ni kiwango cha juu zaidi kwa sasa kinapita kaskazini mwa Puerto Rico.
Zaidi ya nusu ya wakaazi wote milioni tatu wa Puerto Rico hawana umeme baaada ya kimbunga Irma kusababisha mvua kubwa na upepo mkali. Maafiasa wanasema huenda umeme ukakosa kwa siku kadhaa.
Kimbunga hicho chenye nguvu nyingi kuwai kushuhudiwa kwa miongo kadha kilikuwa na upepo wa kasi ya kilomita 295 kwa saa na kilitarajiwa kupita karibu na kwenye pwani cha Jamhuri wa Dominica leo Alhamisi.
Kimbunga Irma kwanza kilikumba kisiwa cha Antigua na Barbuda. Takriban mtu mmoja aliripotiwa kuuliwa ambapo waziri mkuu Gaston Brown alisema kuwa karibu asilimia 95 ya majengo yaliharibiwa.
No comments:
Post a Comment