Wednesday, September 6, 2017

Wajumbe wa bodi migodi ya almasi kikaangoni

Dodoma. Kamati ya Bunge iliyoundwa kuchunguza biashara ya madini ya almasi imependekeza wajumbe wote wa bodi na waliohusika na kusimamia mgodi wa madini hayo, wahojiwe na ikibainika wamehusika mapungufu wachukuliwe hatua.

Akisoma ripoti ya kamati hiyo ambayo itakabidhiwa kwa Spika wa Bunge Job Ndugai ambaye ataikabidhi kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, mwenyekiti wa kamati hiyo, Mussa Zungu amesema wamebaini madudu mengi.

Madudu hayo ni pamoja na upotevu wa kodi, kutosimamiwa vyema kwa uchimbaji wa madini hayo, tofauti kubwa kati ya takwimu zinazotolewa na taasisi za Serikali juu ya kiasi kilichopatikana na kuuzwa cha madini hayo na udanganyifu kuhusu hali na gharama za mitambo.

"Serikali ihoji wajumbe wa bodi na wote ya migodi hii na wote wanaohusika na ikibainika kuwa walihusika katika mapungufu waliyoyaona wachukuliwe hatua,"amesema

No comments: