Mfumuko wa bei wa taifa kwa mwezi Juni, 2018 umepungua hadi kufikia asilimia 3.4 ikilinganishwa na asilimia 3.6 ilivyokuwa mwezi mei, 2018"
Akizuungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), amesema kuwa hali hiyo inatokana na kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Juni mwaka huu kupungua ikilinganisha na kasi ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Mei mwaka huu.
"Kupungua kwa mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Juni mwaka huu kumechangiwa na kupungua kwa mfumuko wa bei kwa baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula" amesema Kwasigabo.
Amefafanua kuwa baadhi ya bidhaa hizo zisizo za vyakula zilizochangia kupungua kwa mfumuko wa bei ni bia asilimia 1.1, gharama za ukarabati wa vifaa vya umeme na viyoyozi kwa asilimia 1.8, gesi za kupikia majumbani kwa asilimia 5.6.
Bidhaa nyengine zilizochangia ni majiko ya mkaa kwa asilimia 2, gharama za mawasiliano kwa asilimia 2.6.
Aidha Kwasigabo ameeleza kuwa mfumuko wa bei kwa baadhi ya Nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Uganda kwa mwaka ulioishia mwezi Juni umeongezeka na kufikia asilimia 2.2 kutoka asilimia 1.7
Kwa upande wa kenya mfumuko wa bei umeongezeka hadi kufikia asilimia 4.28 kutoka asilimia 3.95 kwa mwaka ulioishia mwezi Mei mwaka huu.

No comments:
Post a Comment