Wapigaji mbizi kaskazini mwa Thailand wamewaokoa wavulana wanne zaidi kutoka pango lililofurika maji, duru katika operesheni hiyo ya uokokozi ameiambia BBC.
Hii inaashiria kuwa kwa jumla, wavulana 8 wameokolewa salama huku watu watano wakiwa bado wamesalia ndani ya pango.
Vijana hao 12 na kocha wao wa soka walikwama ndani ya pango tangu Juni 23 baada ya mvua kubwa kusababihsa mafuriko.
Hakujakuwa na uthibitisho rasmi kutoka kwa wanajeshi wa majini wa Thailand wanaoongoza operesheni hiyo kuwa kuna mtu yoyte aliyetolewa salama Jumatatu ikiwa ni siku ya pili katika operesheni hiyo ngumu.
Wavulana 4 waliokolewa salama kutoka pangoni siku ya Jumapili.
Lakini operasheni hiyo ilisitishwa usiku ili mitungi ya hewa ya kusaidia kupumua ipate kujazwa.
Wakoaji waliamua kuendelea na oparesheni hiyo hatari kuwaokoa kufuatia hofu kuwa huenda maji yangeongezeka tena.
Mamilioni ya lita za maji yamekwisha kutolewa kutoka ndani ya pango hilo,ili kurahisisha kazi ya uokoaji.
Kazi hiyo inaharakishwa kufuatia utabiri wa hali ya hewa unaodai kwamba huenda mvua kubwa itanyesha jambo ambalo litasababisha ugumu wa kazi ya kuwaokoa watoto hao.

No comments:
Post a Comment