Wednesday, August 29, 2018

Prof Ndalichako ataka weledi utumike kwenye usahihishaji wa mitihani


WAZIRI  wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako ametoa wito kwa baraza jipya la mitihani kuhakikisha ubora unaotakiwa, usimamizi na usahihishaji wa mitihani unafanyika vyema kwa weledi wa  hali ya juu.

Hayo ameyaeleza leo wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa Bodi ya  Baraza la Mitihani nchini ambapo  amempongeza pia mwenyekiti wake Prof. William Anangisye aliyeteuliwa Julai  mwaka huu na Rais  John Magufuli.

Prof. Ndalichako amewatakia mitihani mema wanafunzi kote nchini wanaotarajiwa kuanza mitihani yao Septemba mwaka huu, lakini akatoa angalizo kwa walimu waliojipanga kufanya udanganyifu wa mitihani kuwa watachukuliwa hatua kali.

“Kwa kuzingatia hilo, ni imani yangu kuwa baraza hili litahakikisha malengo yake yanafikiwa,” alisema na kuwapongeza wote waliohusika katika kuhakiki vyeti vya watumishi wa umma nchini kwa uaminifu.

No comments: