Monday, August 6, 2018

Waziri Ummy aahidi serikali kupanua vyuo vya afya


WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema wizara yake itaendelea kukarabati na kupanua vyuo vya mafunzo ya afya kada ya kati nchini ili kuweza kuongeza udahili kwa wanafunzi wanaofaulu kwenye masomo ya sekondari wenye vigezo vya kuingia kwenye vyuo hivyo.

Aliyasemma hayo leo wakati halfa ya uzinduzi na makabidhiano ya Majengo ya chuo cha Uuguzi Tanga yaliyojengwa kupitia ufadhili wa mfuko wa Dunia wa Kupambana na Ukimwi Kifua Kikuu na Malaria (Global Fund) alisema kwani ukarabati huo utasaidia kuongeza idadi kubwa ya wanafunzi watakaokuwa wakipata fursa ya kusoma kwenye vyuo hivyo.

Alisema kutokana na ukarabati huo kwenye chuo cha Uuguzi mkoani Tanga idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa kwenye chuo hicho imeongezeka kutoka wanafunzi kutoka 190 hadi 260 ambao wameweza kupata fursa mafunzo kwenye chuo hicho ambao watasaidia kwenye kada hiyo muhimu kwa ustawi wa maendeleo.

“Kutokana na ukarabati wa majengo haya nimeambiwa na Mkuu wa Chuo kwamba udahili wa wanafunzi kutoka 190 hadi 260 wameweza kutoa fursa kwa vijana wao kuweza kupata nafasi ya kupata mafunzo ya afya kada ya kati huwa naambiwa kwamba na dkt Guwele ambaye ni mkuu wa idara ya mafunzo na afya kada ya kati anasema wanafunzi wengi wanafaulu lakini hawapati mahali pa kuwapeleka sababu kubwa zikiwa ni miundombinu na uchakavu wa majengo na inaumiza vijana wamefaulu vizuri sana lakini hakuna nafasi“Alisema.

“Lakini tunawashukuru Global Fund kwa ujenzi wa majengo hayo yameweza kusaidia kuongeza udahili hivyo niagize msije mkaacha wanafunzi kwa kusema hakuna nafasi..Wanafunzi waliofaulu kwenye masomo ya sekondari wenye vigezo vya kuingia kwenye vyuo vya mafunzo wachukuliwe wote wasiachwe majumbani “Alisema.

No comments: