Saturday, January 5, 2013

KANDORO AZINDUA CHANJO YA ROTAVIRUS NA NIMONIA KATIKA KITUO CHA AFYA RUANDA MBEYA


Mkuu wa mkoa Mbeya Abass Kandoro akikata utepe kuzindua chanjo ya mpya ya Rotavitus na Nimonia katika kituo cha afya Ruannda jijini Mbeya
Mkuu wa mkoa Mbeya Abasi Kandoro akimwekeamatone moja ya watoto waliyofika katika uzinduzi huo
Mkuu wa mkoa Mbeya akihutubia wananchi waliyofika katika uzinduzi wa chanjo hiyo
Mratibu wa chanjo mkoa wa Mbeya Japhet Mihanye akisoma risala kwa mgeni rasmi
Mstahiki meya wa jiji la Mbeya Atanath Kapunga akimshukuru mgeni rasmi kwa uzinduzi wa chanjo hiyo
Baadhi ya wakina  mama waliyobahatika kupata chanjo katika uzinduzi  leo
Uzinduzi wa leo unaongeza harakati za serikali za kupambana na adui maradhi hususani maradhi yanayozuilika kwa chanjo na hiyo kufikia malengo ya milenia namba 4 ambayo ni kupunguza vifo vitokanavyo na maradhi kuharisha na nimonia lengo hili linatakiwa liwe limefikiwa ifikapo mwaka 2015

picha na mbeya yetu

Waziri Membe atangaza kutogombea ubunge tena

Bernard-Membe14 d0bb1
WAZIRI wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ametangaza kuwa hatogomea tena ubunge katika uchaguzi mkuu ujao.Membe ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mtama, mkoani Lindi, alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza kwenye sherehe za Mwaka Mpya nyumbani kwake.

kinana akemea chokochoko za kidini

kinana 948a8
KATIBU Mkuu wa CCM,Abdulrahman Kinana amekerwa na chokochoko za kidini zilizoanza kujipenyeza hivi karibuhi na kutoa wito kwa madhehebu ya dini na taasisi zake hapa nchini,kuendelea kuhubiri amani kwa kuliombea taifa , ili wananchi waendelee kujivunia amani iliyoachwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.
Kinana alitoa kauli hiyo juzi kwenye maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Imam Husein, yanayoadhimishwa na dhehebu la KhojaShia Ithna Asheri Jamaat Arusha kote duniani na kufanyika kwenye msikiti wa jumuiya hiyo jijini hapa , ambapo watu mbalimbali wakiwamo viongozi wa madhehemu pamoja na viongozi wa chama na Serikali walihudhuria.
Kinana alisema kuwa upo umuhimu mkubwa kwa viongozi wa dini na taasisi zake kuendelea kuienzi amani kwa kuhubiri suala la kudumisha amani na kuonya kwamba Serikali haitasita kuchukua hatua za haraka kwa mtu ama kikundi chochote cha dini kitakachojihusisha na uvunjivu wa amani.

DK. HARRISON MWAKYEMBE ATEMBELEA UWANJA WA NDEGE SONGWE MBEYA

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege(TAA) Mhandisi Suleiman S. Suleiman akimwelezea Dk Harrison Mwakyembe jinsi uwanja wa ndege songwe unavyofanya kazi toka uzinduliwe mwezi wa 12 mwaka jana na kuwa sasa uwanja huo umebaki maendeo ya maegesho ya ndege kubwa kama boing 737 

Mmoja ya wahandisi wa ujenzi wa uwanja huo wa songwe akimwelezea waziri wa uchukuzi Dk Mwakyembe  akimwelezea hatuza za mwisho za ujenzi wa maegesho  ya ndege kubwa
Mkuu wa majeshi Tanzani Jenerali Mwamnyange akisalimiana na kuagana na RPC wa Mbeya Diwani katika kiwanja hicho cha songwe kabla ya kuanza kwa ziara ya waziri wa uchukuzi Dk Mwakyembe 
Jenerali Mwamnyange akiondoka uwanjani hapo kurejea Dsm alikuwepo Mbeya kwa mapumziko Mafupi
Huu ni mnara  wa kuongozea ndege katika kiwanja hicho cha Songwe Mbeya
Mwongoza ndege mwandamizi John Chambo akimwezea waziri Mwakyembe jinsi wananvyofanya kazi ya kuongoza ndege katika mnara huo
Mkuu wa kitengo cha hali ya hewa Issa Hamad akimwelezea waziri mwakyembe juu ya shughuli zoa za upimaji wa hali ya hewa uwanjani hapo na mkoa kwa ujumla kuwa 
Hili ndilo eneo la maegesho ya ndege kubwa aina ya boing 737 ambalo mwishoni mwamwezi huu wa kwanza litakamilika
Hili ni eneo la kutua ndege na kurukia  barabara hiyo ya ndege inaurefu wa zaidi ya kilometa 3.5 km
Hii ni sura ya mbele ya uwanja huo wa songwe Mbeya
Hili ni jengo la kikosi cha zimamoto uwanjani hapo
Hawa ni waandishi wa habari walioanza kuripoti ujenzi wa uwanja huo tangu unaanza kujengwa mpaka sasa kulia kabisa  Chales Mwakipesile Brand Nelson Felix Mwakyembe na Joseph Mwaisango inaelekea kuna kitu wanashangaa
Waziri wa uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza ziara yake katika uwanja huo wa songwe amesema kuwa uwanja wa Songwe wa kimataifa ni kati ya viwanja vikubwa viwili kujengwa baada ya uhuru ukitanguliwa na uwanja wa Mkoa wa Kilimanjaro kwani viwanja vingine vimekuwa vikifanyiwa marekebisho                                                                                                                        Tumeanzisha historia mpya kwani dunia inafahamau kwa sasa kuna uwanja wa kimataiafa wa Songwe, upo wazi umekamilika na umeanza kutumika alisema
Picha na Mbeya yetu
Post a Comment