Wednesday, January 2, 2013

Juma Kilowoko ‘Sajuki’ Amefariki Dunia Leo Alfajiri

 


Simon Mwakifwamba (kushoto) na wadau wengine wakimsaidia Sajuki (katikati) kutoka jukwaani baada ya kudondoka katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha mwishoni mwa mwaka jana.
STAA wa filamu za Kibongo, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ amefariki dunia leo alfajiri katika hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa anapatiwa matibabu. Kwa mujibu wa Katibu wa chama cha waongoza Filamu Wilaya ya Ilala, Rajabu Amiri ni kwamba hivi karibuni Sajuki alikuwa anasumbuliwa na tatizo la upungufu wa damu. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amen!

Leo Jumatano

IMG-20130102-00126 cdd25

MICHEZO

MFARANSA WA SIMBA AAHIDI KUVUNJA REKODI YA SIANG'A 2003 SIMBA SC

Liewig kushoto akisaini mkataba jana. Kulia Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Nyange 'Kaburu'

Na Mahmoud Zubeiry
KOCHA mpya wa Simba SC, Mfaransa Patrick Liewig amesema kwamba lengo lake ni kuifikisha klabu hiyo katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka huu na anaamini hilo linawezekana kwa kuwa timu ina wachezaji wazuri.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana, Liewig alisema kwamba ana imani Simba ni timu nzuri, kwa sababu katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kilichoifunga 1-0 Zambia, kulikuwa kuna wachezaji wengi wa Simba SC.
“Zambia ni timu nzuri, ni mabingwa wa Afrika, kama Tanzania iliifunga Zambia ikiwa na wachezaji wengi wa Simba, sioni kwa nini tusifike Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa,”alisema Liewig.
Liewig alisema leo anakwenda Zanzibar kuungana na kikosi cha timu hiyo ambacho kitakuwa kikishiriki Kombe la Mapinduzi.
“Nitakutana na wenzangu katika benchi la ufundi huko, Julio (Jamhuri Kihwelo) na Moses (Basena), tutashirikiana kufanya kazi, baada ya hapo tutakwenda Oman, tukirudi tutaanza Ligi (Kuu) na Ligi ya Mabingwa.
Nimeambiwa pia kuna Kombe la Kagame (Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati) Rwanda, tutakwenda, pamoja na yote, nitashughulikia pia na program ya vijana, lazima tuibue vipaji kutoka chini,”alisema.  
Simba SC itaanza na Recreativo de Libolo ya Angola, katika Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Februari 17 hadi 19 na kurudiana nayo kati ya Machi 2 na 4, mwakani.
Mara ya mwisho Simba SC kucheza hatua ya makundi ya michuano hiyo ilikuwa mwaka 2003, wakati huo ikiwa chini ya kocha Mkenya, James Aggrey Siang'a.
Liewig jana alisaini mkataba wa miezi 18 kuifundisha Simba, akimpokea Mserbia Milovan Cirkovick aliyetupiwa virago baada ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Bara. 
Liewig ni kocha wa zamani wa Akademi ya Paris Saint Germain (PSG) ya Ufaransa, ASEC Mimosas ya Ivory Coast na Club Africain ya Tunisia, ambaye ana Stashahada ya Juu ya ukocha na Shahada ya tatu ya ualimu wa soka ya vijana aliyotunukiwa na Mkurugenzi wa Ufundi wa Ufaransa, Gerard Houiller, anatarajiwa kwenda Zanzibar kesho.
Liewig pia amehudhuria kozi za ufundishaji mazoezi ya viungo Juni mwaka 1999 katika Chuo Kikuu cha Dijon.
Kwa upande wa uzoefu, Liewig alifanya kazi PSG kuanzia mwaka 1989 hadi 1999 kama Kocha Mkuu wa akademi na kuna wakati alikuwa akishirikishwa pia katika programu za timu A, ingawa majukumu yake zaidi yalikuwa ni kwa Under 20, Under 18 aliowawezesha kutwaa Kombe la French Junior Gambardella na Under 16.
Kuanzia mwaka 1989 hadi 1990:  alikuwa Meneja Mkuu wa Tomislav IVIC, 1990 hadi 1991 alikuwa Msaidizi wa Henri Michel, 1991 hadi 1994 alikuwa Msaidizi wa Artur Jorge, 1994 hadi 1996 alikuwa Msaidizi wa Luis Fernandez, 1996 hadi 1998: alikuwa Msaidizi wa Ricardo Gomez, 1998 hadi 1999 alikuwa Msaidizi wa Alain Giresse.
Liewig pia alifundisha Al Wahda FC ya Abu Dhabi kuanzia 1999 hadi 2001, ambayo aliipa ubingwa wa Ligi Kuu ya nchi hiyo na Kombe la Ligi.
Januari mwaka 2003 alikuwa Msimamizi wa Chama cha Soka UAE katika fainali za Afrika za U20 nchini Burkina Faso.
Kuanzia mwaka 2004 hadi 2009 alikuwa Kocha wa ASEC Mimosas ya Ivory Coast aliyoipa mataji matatu ya Ligi Kuu ya nchini humo mfululizo, 2004, 2005 na 2006, Super Cup ya nchini humo 2005, 2007, 2008 na 2009 na akaiwezesha kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa mara tatu, mara moja akiifikisha Nusu Fainali.
Amekuwa Kocha bora wa Ivory Coast miaka mitatu mfululizo, 2004, 2005 na 2006 na tangu Septemba mwaka jana hadi Juni mwaka huu, alikuwa kocha wa Club Africain ya Tunisia

JK.Azindua Matokeo Ya Sensa Ya Watu Na Makazi 2012.

Rais Jakaya Kikwete akibonyeza kitufe kwenye kompyuta kuzindua matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi mwaka 2012  jana jijini Dar es salaam ambapo idadi ya watu Tanzania imefikia milioni 44 929 002. Picha na Aron Msigwa -MAELEZO

Rais Jakaya Kikwete katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa serikali na vyama vya siasa.


Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja  kwenye bango linaloonyesha idadi ya watu Tanzania na viongozi na watendaji wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu mara baada ya kutangazwa kwa matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012.

No comments: