|
MAREHEMU GABRIEL MWASYEBULE ENZI ZA UHAI WAKE |
|
WANANCHI WA LWANGWA NA VITONGOJI YAKE WAKIWA WAMEMPIGA MAREHEMU GABRIEL MWASYEBULE HADI KUUA NA KUMCHOMA MOTO |
|
KAMERA YA KINGOTANZANIA ILIFANIKIWA KUFIKA KWENYE TUKIA MUDA WA SAA NANE BILA YA KUSHUHUDIA MTU YEYOTE WOTE WAKIWA WAMEJIFICHA KWA KUOGOPA KUKAMATWA NA VYOMBO VYA DORA. HAPO NI MHE DIWANI ALIPOKUWA ANASHUHUDIA MAUAJI YALIVYOFANYIKA |
|
SAA KUMI NA MBILI ASKALI POLISI WALIFIKA ENEO LA TUKIO NA KUUONDOA MWILI WA MAREHEMU ENEO LA UKIO NA KWENDA NAO TUKUYU KWA AJILI YA KUFANYA UCHUNGUZI KABLA YA KUKABIDHIWA NDUGU |
|
KULIA NI MWENYEKITI WA KIJIJI CHA IKAMA MBANDE GWAKISA MWANDEMELE AKIWA NA MHE DIWANI AKIELEZA TUKIO LA MAUAJI LILIVYOTOKEA. GWAKISA AMESEMA KUWA TANGU ASUBUHI WATU WENGI WA KILA PANDE WALIKUSANYIKA KATIKA UWANJA WA MBADE NA KUSUBIRI VIONGOZI KWAMAANA YA CHUFU ANDINDI MWAKALOBO KWENYE MKUTANO WA HADHARA AJE ATOE MAELEKEZO KUHUSIANA NA TUKIO LA UCHAWI LINALOENDELEA. TOFAUTI NA MATARAJIO YA WENGI NI PALE CHIFU ANDINDI MWAKALOBO ALIPOHAIRISHA MKUTANO NA KUWATANGAZIA WANANCHI WAKE KUWA KIKAO HAKIPO HUKU WANANCHI WAKITEGEMEO KUMUONA MCHAWI WAO NA VITU VYAKE VYA KICHAWI, MAKUTANO MKUBWA UKAMZOMEA NA KUMSONGA CHIFU KUWA KALA RUSHWA KUTOKA KWA MHUSIKA, NDIPO VIJANA NA WENGINE WAKAAMUA KWENDA KIJIJI CHA NDEMBO AMBAKO NDIKO ALIPOKUWA GABRIEL NA KUAMUA KUMLETA MKUTANONI LAKINI WALIPOFIKA NYUMBANI PAMOJA NA KUMKOSA WALIAMUA KUVUNJA MILANGO WAKIDHANI AMEJIFICHA LAKINI MWISHO WA SIKU WALIKIFANIKIWA KUMKUTA POLINI AKIWA AMEJIFICHA NA KUMKAMATA NA KABLA YA KUMFIKISHA UWANJANI WALIAMUA KUMPIGA HADI KIFO NA KUMCHOMA MOTO. |
|
MAREHEMU AKIPAKIWA KWENYE GALI TAYARI KUMPEREKA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI TUKUYU UKISUBIRIWA UCHUNGUZI |
|
NYUMBA YA MAREHEMU GABRIEL MWASYEBULE ANAYOTUHUMIWA KUIJENGA KWA UCHAWI |
|
MOJA YA SHAMBA LA VIAZI VINAVYO SUBIRIWA KUVUNWA MWEZI HUU, SHAMBA LA MAREHEMU GABRIEL MWASYEBULE, MASHAMBA AMABAYO PIA NI MOJA YA SABABU AMBAZO WANANCHI WA LWANGWA WANAMTUHUMU MAREHEMU KUWA ALIKUWA ANAWALIMISHA WATU KIUCHAWI NA KUIBA MAZAO YA MASHAMBA MENGINE KIUCHAWI ILI SHAMBA LAKE LIWE NA MAZAO MENGI NA MAZURI |
|
HII NDIO STOO YA KUWEKEA MAZAO MBALIMBALI AMBAYO MAREHEMU ALIKUWA ANATUMIA KUTUNZIA MAZAO YAKE KATIKA MISIMU MBALIMBALI KAMA MAHINDI , NYANYA NA VIAZI. |
|
BAADA YA MAUAJI KUFANYIKA KAMERA YA KINGOTANZANIA IMESHUHUDIA VIJANA WENGI WA LWANGWA NA VIJIJI VYAKE KUTOLOKEA KUSIKO JULIKANA WAKIHOFIA KUKAMATWA NA POLISI |
|
BAADA YA KUUSILIRI MWILI WA MAREHEMU KWENYE JENEZA HAPA NDUGU WAKITOKA NA NA JENEZA LA MAREHEMU GABRIEL MWASYEBULE KATIKA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI KATIKA HOSPITAL YA WILAYA TUKUYU NA KUELEKEA SEHEMU YA MAZIKO KIJIJINI KWAO NDEMBO LWANGWA |
|
NDUGU NA JAMAA WAKISHIRIKI MAZIKO YA GABRIEL MWASYEBULE KIJIJINI KWAO NDEMBO LWANGWA |
|
JENEZA LA MWILI WA MAREHEMU LIKIINGIZWA KABURINI |
|
BAADHI YA WANAKIJIJI NA NDUGU WAKISHIRIKI MAZIKO YA MAREHEMU GABRIEL MWASYEBULE |
|
BABA MDOGO WA MAREHEMU AKIONGEA BAADA YA MAZIKO , AKIWASHUKURU WANANCHI WALIOFIKA KUHUDHULIA MAZIKO YA MWANAE ALIYEUWAWA NA WATU KWA TUHUMA ZA KUWA MCHAWI. HUKU AKIWAPA TAARIFA ZA KIKAO CHA FAMILIA KILICHOKAA SIKU MOJA KABLA YA TUKIO LA MAUAJI AMBAPO FAMILIA YOTE ILIKAA NA MKUSIKA KUULIZWA KAMA ANAHUSIKA NA TUHUMA ZA UCHAWI ZINAZOONGELEWA NA WATU AMA HAUSIKI LAKINI BAADA YA MAULIZANO YA MUDA MLEFU SANA MAREHEMU GABRIEL MWASYEBULE ALIKATAA KUWA HANA UCHAWI WOWOTE ULE ILA NI MAMBO AMBAYO YANATENGENEZWA ILI ACHAFUKE ASIFIKIE MAFANIKIO YAKE YA MAISHA. NDIO YALIKUWA MANENO YA FAMILIA YA MWASYEBULE KATIKA MAZIKO NA KUWATAKA FAMILIA KUWA WATULIVU KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU SANA |
MATUKIO
ya kujichukulia sheria mikononi bado yanazidi kuyakumba baadhi ya
maeneo mkoani Mbeya ambapo katika tukio hili kijana Gabriel Mwasyebule
miaka 39 ameuawa na wananchi wenye hasira kali wakimtuhumu kwa imani za kishirikina.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi,
amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kumtaja marehemu liyetambulika
kwa jina la Gabriel Mwandemwa (Mwasyebule) mkazi wa kijiji cha Ikamambande
(Lwangwa) Wilaya ya Rungwe aliuawa na watu wasiofahamika kwa kukatwa na vitu
vyenye ncha
kali sehemu za kichwani na kifuani.
Alisema tukio hilo lilitokea siku ya jumapili majira ya saa tano
asubuhi huko katika Kijiji cha Ikamambande, kata ya Lwangwa, Tarafa ya
Busokelo, Wilaya ya Rungwe, mkoaniMbeya
Alisema taarifa za awali zinadaiwa kuwa, uongozi
wa kimila kijijini hapo uliitisha kikao
cha dharura ukihusisha viongozi wa vitongoji na vijiji jirani na ndipo waliamua
kumtafuta na kumlazimisha marehemu kuhudhuria katika kikao hicho na kisha
kuanza kumpiga na kupelekea kifo chake.
Alisema marehemu alikuwa akituhumiwa kuwa ni
mshirikina kijijini hapo kwa kuwa anawaroga watoto na kuwa anajipatia mazao
mengi ya mavuno ya viazi na kujipatia pesa zilizowezesha ujenzi wa nyumba yake aliyoweka malumalu na Gipsam pia kumiriki pikipiki moja huku akitarajia baada ya mavuno mazuri ya mwaka huu kununua gali la kutembelea.
KINGOTANZANIA - 0752881456
No comments:
Post a Comment